MWANAMKE KWA JINSIA NI YULE YULE tofauti ya Mwanamke wa zamani na Mwanamke wa sasa ni MABADILIKO YA TABIA DUNIA💃
Pamoja na hilo la mabadiliko lakini nilichojifunza ni kwamba WANAUME WAMEKALILI KWAMBA ZAMANI NDO KULIKUWA NA WANAWAKE eti sasa hakuna Wanawake ila sijui wanawaitaje wenyeee🤣
NISIKILIZE MWANAUME;
Utambue kwamba hata wanaume wa zamani "BABU NA BABA ZETU" Waliwapenda wake zao, Mwanaume wa zamani alioa wanawake watatu ama zaidi lakini kila mmoja alikuwa na SHAMBA, NYUMBA, MIFUGO na mengineyo mengi, Wanaume wa zamani walihakikisha mkewe anayo mahitaji yote ndipo wakaenda kucheza BAO... Mwanaume wa zamani alimpa Uhuru mkewe, Mwanaume wa zamani alihakikisha Mke ndiye mlinzi wa familia, Sasa wewe ndugu yangu hujui mke anakula nini? Hujui mtoto analipiwa ada shilingi ngapi BADO UMLALAMIKIE MWANAMKE WA SASA? Hebu nikukumbushe jambo "ZAMANI MWANAMKE AKIWA NA KITENGE CHA WAX NDO WA KISHUA JE UNAJUA WANAWAKE WA LEO KITENGE WANAENDEA MISIBANI?"
Kama ndo hivyo kubaliana na mabadiliko ya TABIA DUNIA! Usimchukue mtoto wa watu akawe Mke wako kwa kutaka awe kama Bi'mkubwa alivyokuwa.... Hizi ni zama mpya, Enzi zile Mama zetu anaishi na MUME wa Elimu ya darasa la 4 wakati huo yeye hata kusoma hajui, Leo kabinti ka miaka 22 ni ka daktari BADO UNATAKA KULAZIMISHA WANAWAKE WA SASA WAWE KAMA WA KALE? Hebu Acha hizo ndugu yangu, Kwanza Wanaume tusipoangalia TUNAKWENDA KUKOSA HESHIMA bali tutapewa THAMANI YA MBEGU ZETU TU🙆🏿♂
Hujawahi kuona Mwanamke anazaa na Mwanaume na hampendi? Jiongeze Man💪🏽 Kubaliana na Mazingira pamoja na nyakati, Mwanamke wa zamani ni huyu huyu wa sasa ni DUNIA KUBADILIKA hivyo uendane na DUNIA KWA KILA KITU sio ukatae kulala kwenye Matembe ila utake Mkeo afuate mambo ya kale🕺
#Elista_kasema_ila_Sio_she
Post a Comment