Safari yako ya maisha haiishii kwenye usichana, bali usichana ndo mwendelezo wa umwanamke wako hata kufikia kuwa MAMA.
Wakati ambao kifua kitakuwa saa 6, Wakati ambao utakuwa bikira, Wakati ambao kila kiungo mwilini mwako hakijakomaa, Kumbuka kuna wakati Kifuani utakuwa ukivaa blazia, Bikira haitakuwepo, Maungo yako kulegea na hapo ndipo nataka ujue ndipo pa kuanzia kuutafuta mwisho wako mwema.
Wakati ambao ndo unatakiwa kuchagua BABA WA WATOTO 👪WAKO kwani hilo ndilo la muhimu kuliko kuchagua MUME KWA AJILI YAKO.
Kwanza kabisa tambuwa uwapo MSICHANA unakuwa kwenye JOTO♨ kali la wanaume kukuhitaji kuliko utakapokuwa umekuwa MAMA.
Haimaanishi kwamba ukizaa utakosa mvuto laa hasha bali nazungumzia JOTO♨ Yaani usichana ni sehemu ambako UPO MOTO🔥 unaweza kuwavutia wanaume 100 Kwa wakati mmoja, kuliko ukiishakuwa Mama utawavutia wachache wanaoendana na mahitaji yao kwako kwa wakati huo.
Baada ya USICHANA👱 wako ni wewe kuwa MAMA👪 na hilo ndilo ambalo nakushauri leo, Kuwa na MUME haimaanishi umepata BABA wa UZAO wa TUMBO lako, Kwa sababu sio kila MUME ALIYE NA MKE ANAJUA WAJIBU WAKE KWA WATOTO WAKE achilia mbali kwa familia yake, Kwa sasa ni kama FASHION ukiwa na kazi, ama kipato chako usiamini sana kwamba MUME anayekuoa atakuwa BABA Kwani wengi wao wanapenda CHEO CHA MUME lakini kusimama kama BABA ndo bahati nasibu, Mwanamke tambuwa kwa sasa WANAUME wanapenda KUBET NDOA kuliko hata KUOA.
Wanawake kwa wingi wenu mjikumbushe MAHANGAIKO mnayopitia baada ya kuolewa, Sio WENYE VIPATO VYA CHINI, VIPATO VYA KATI, MATAJIRI wote mnalia kilio kimoja kosa ni Mwanaume kujua MKE ANAO UWEZO WA KUTUNZA FAMILIA hapo mwanangu imekula kwako😅😅😅😅
Ndo maana nasisitiza kwamba;
▪UCHAGUE BABA WA WATOTO WAKO BADALA YA KICHAGUA MUME.
MUME anaweza kuwa sehemu ya burudani na amani ya MOYO wako lakini asijue kuwajali watoto wako, lakini ukichagua BABA WA WATOTO WAKO akiwafurahisha watoto wako hata wewe UMEFURAHI NA KUPATA AMANI YA KUDUMU.
Wachana na viji furaha na amani vya mpito pengine unavichangiza kwa kumpa kitu mwanaume mwisho wako ni mbaya uwapo na MUME badala kuwa na BABA WA WATOTO WAKO Sina maana Baba mmwaga mbegu laaa hashaaa namzungumzia BABA AJUAYE MAJUKUMU YAKE KAMA BABA KWA WANAYE💪
#Elista_Kasema_ila_Sio_She
Post a Comment