MWANAMKE ITAMBUE NAFASI YAKO KATIKA NDOA NA NAMNA UNAVYOWEZA KUMDHIBITI MMEO ASICHEPUKE.

Image may contain: 2 people

Hata simba ni mkali mno porini ila mwisho wa siku nae ana fall in love na simba jike, anapewa kitu roho inapenda na kuzaliwa watoto, jambo hili ni kama masihara ila ukweli unabaki kuwa hayo ndio mapenzi.

Mwanaume yeyote chini ya jua udhaifu wake kwa namna moja au nyingine upo chini ya mwanamke hakika hata manabii wakubwa akiwemo Daudi(Mfalme Daud), Suleiman, Samson na wengineo walijikuta pamoja na imani zao kubwa na hadhi zao ila mwisho wa siku walijikuta wakiangukia mikononi mwa mwanamke.
Wapo wanawake waliozitumia nafasi zao kuwatawala na kuwapotosha waume zao ila leo ninazungumzia ni jinsi gani mwanamke anaejitambua vyema anaweza kutumia nafasi yake vyema kumdhibiti mme wake katika ndoa.

Mwanaume huwa ni kama bendera, anafuata upepo. Upepo huo unaundwa na mapenzi moto moto yaliyotawaliwa na ubunifu, usafi, unyenyekevu, uvumilivu, heshima, uaminifu, usikivu, utii, upole, ukarimu, upendo wa dhati, shukrani, hofu ya Mungu na tabia njema

Mwanamke jitambue nafasi yako kuhakikisha unakua na upepo mkali utaomudu kupeperusha hiyo bendera yako(mmeo) huko ndani kisawasawa. Maana iwapo ukizembea utakuta bendera ishashuka mlingoti imeanguka matopeni tayari mabaamedi, mashangingi, makahaba na mashoga wa saloon washakuibia mme, kwa hiyo JIPANGE BIBI.
Mumeo ndio mfalme wako na wewe ni malikia wake hakikisha unatimiza majukumu yako ya kimalikia usizubae hadi vijakazi wako wakalala na mfalme.

Kabla hujaulizia ni nani MCHAWI WAKO anaechupuka na mme wako tafakari ni kwa kiasi gani unatimiza majukumu yako ya kindoa na je unahisi nini alichokimisi kwako hadi akakitafute nje HAKIKA UTAGUNDUA MCHAWI NI WEWE MWENYEWE

Mdhibiti mmeo kirahisi kabisa, fanya haya:
#muombee Mungu amlinde
#mfariji
#mkarimu
#mshauri, mtii, mheshimu
#sali nae atakua na hofu ya Mungu hatothubutu kufikiria kusaliti ndoa
#mpe mawazo ya kimaendeleo
#msafi
#mlishe, muogeshe, mvishe na kumsifia
#umbembeleze
#mpikie chakula kitamu
#jitume chumbani na ubunifu
#jisafi, jipambe, nukia, mchombeze

Hakika kwa yote hayo akichepuka bado ACHANA NAE huyo UZIN-ZI NI TABIA YAKE.

Kama umenielewa sema "IMEPENYA HIYO" kisha share post hii na marafiki zako wapate funzo hili.

Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post