☑️ MWANAMKE BORA HANUNULIKI NG'OO NA SIO KWAMBA HAWAPO 👈WAPO KIBAO


Kuna watu (mimi nawaita wahuni wa mjini) huamini na kusema kwamba WANAWAKE wote wananunulika bila kujali umri, cheo ama status ya ndoa:- mradi ufike "bei" inayomtosha "unambeba". Awali nilikuwa nikikasirika sana ninaposikia kauli yao hiyo, lakini baada ya utafiti nikagundua kwamba wako sahihi sana wanaposema "kila MWANAMKE ana bei yake". Katika bei zilizopo sokoni kuna WANAWAKE ambao bei zao hazina ukomo (yaani infinite price) kiasi kwamba hakuna kiwango unachoweza kuwa nacho hapa duniani kikatosha kuwanunua. Hawa WANAWAKE wenye "infinite prices" ni wale ambao hawashoboki na fedha, mali, cheo ama umaarufu wa yeyote anaewashawishi kuwasaliti wapenzi na waume zao.
Hawa WANAWAKE wenye "infinite price" ni wale ambao wanajitambua na kuelewa kwamba thamani ya mapenzi haimo katika vitu bali moyo, kwa hiyo huwezi kutumia pesa kama chambo ya kuwapata na kuwatumia kimapenzi. La hashaHawa WANAWAKE "wenye infinite price" ni wale ambao wamemshika MUNGU, wananyenyekea na kuwapenda WAUME zao kwa moyo na hawababaiki kwa lolote:- kiasi kwamba hata ukiwatishia kuwafukuza kazi ikiwa watakunyima mapenzi:- wako radhi kukuachia kazi yako na kwenda zao Ukisikia wahuni wa mjini wanasema kila MWANAMKE ana bei na anaweza kununulika kimapenzi basi ujue wanaongela WANAWAKE wasiojielewa maana wanaojielewa ni wale wenye "infinite prices"


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post