🌳🌲* *MAUMIVU YA TUMBO KIPINDI CHA HEDHI* * 🌲🌳


Fuatana nami katika nakala hii
Kuumwa tumbo wakati wa hedhi
🍀Tumbo la hedhi au maumivu wakati wa hedhi (period pains) au kitaalamu dismenorrhea, ni maumivu yanayojitokeza sehemu ya chini ya tumbo au kiunoni wakati mwanamke anapoanza kupata siku zake au kabla ya hapo. Maumivu hayo huweza kuwa madogo au ya wastani huku baadhi ya wanawake wakipata maumivu makali sana. Maumivu ya tumbo wakati wa hedhi huanza pale mayai yanapotoka katika mirija (fallopian tubes) na kuteremka chini ya mirija hiyo wakati wa Ovulation.
*Maumivu ya tumbo la hedhi yapo ya aina mbili* . 🍀Aina ya kwanza au (Primary Dysmenorrhea) ni maumivu yasiyokuwa na sababu zozote za kimsingi za kitiba. Katika aina hii maumivu ni ya kawaida na huhisiwa sehemu ya chini ya tumbo na kiunoni. Maumivu hayo huanza siku moja au mbili kabla ya hedhi na humalizika baada ya siku mbili au nne.
🍀Aina ya pili au (Secondary Dysmenorrhea) ni yale maumivu yanayojumuisha maumivu yanayosababishwa na sababu nyinginezo za kitiba kama vile matatizo katika kizazi, ugonjwa wa nyonga (PID) na matatizo katika mirija ya mayai.
🍀Takribani nusu ya wanawake wote waliopo katika umri wa kuweza kupata mototo wanakumbana na maumvu wakati wa hedhi, maumivu ambayo huanza siku chache kabla ya hedhi na kuendelea kwa siku kadhaa. Baadhi ya wanawake hupata maumivu ya kawaida lakini kwa wengine maumivu huwa makali sana hadi kupelekea kushindwa kufanya shuguli zao. Hii ni moja ya sababu watoto wa shule kukosa vpindi kwa siku kadhaa. Ili kupata tiba basi wanawake wengi hukimbilia kunywa dawa za kupunguza maumivu na baadhi ya madactari hutoa ushauri wa kunywa vidonge ili kuzuia hedhi ili kupunguza makali ya maumivu, njia zote hizi mbili zikiwa na madhara na pia kutoweza kutoa suluhisho ala kudumu la tatizo husika.
🍀Uchunguzi unaonyesha kuwa kuna sababu mbalimbali zinazoweza kuongeza uwezekano wa kuumwa tumbo wakati wa hedhi.
🌱• Kuwa na umri wa chini ya miaka 20.

No photo description available.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post