MAISHA NI KAMA KUTONGOZA, HUWEZI KUSEMA UMESHINDWA KAMA HUJAJARIBU!

Image result for MAPENZI YA MBALI; HATAKI UENDE KWAKE ANATAKA AJE YEYE KUKUTEMBELEA.
Huwezi kusema umeshindwa kama hujajaribu. Maisha ni kama kutongoza, huwezi kumpata mtu unayemtamani kama hujamuambia kuwa unamtaka. Huwezi kusema yule Dada amenikataa au yule Kaka hanitaki kama hata hujamuuliza. Kuna wanaume huona wanawake wazuri wakawaangalia, wakajiangalia hali zao na kusema hapana yule hawezi kunikubali na hali yangu.
Wanakaa kimya bila kuongea, wanawakosa, lakini pia kuna wanawake wengi huwaona wakaka wazuri na kuwatamani, husishia kusema namtaka lakini siwezi kumuambia hawezi kunikubali mtu kama mimi. Nao huishia katika maumivu na kuwakosa. Lakini kuna wale ambao huona wakatamani na kusema poteli ya mbali, kwani akinikata ndiyo nini.
Huenda kuongea na kumwaga sera zao, wanakubaliwa au kukataliwa lakini mwisho wa siku wamejaribu na hata kama wakikataliwa basi wanakua na uzoefu na wanajenga kujiamini tena. Wanajua ladha ya kujaribu, hivyo unapotamani kufanya kitu cha mafanikio kua kama unatongoza, kama hutajaribu kukifanya basi hutakipata lakini ukijaribu unaweza kukipata au ukakosa!
Huwezi kusema biashara flani ni ngumu, haina faida kama hujawahi kuifanya, kuna watu wengi ambao wamefanikiwa kwa kitu ambacho unakiona kama hakiwezekani. Najua uwezi kufanya kila kitu lakini nilazima ufanye kitu kama unataka hali yako ya maisha kubadilika, nilazima uchukue hatua flani na ufanye jambo flani. Hembu anza sasa kwa kuondoa akilini neno haiwezekani na kaunza kuwaza inawezekana, tafuta namna!


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post