BWANA mmoja aliwaitisha wanawe wanne, na kuwapa somo juu ya kujifunza kutokuhukumu mambo kwa haraka.
Akawataka waende, kwa awamu, nchi moja ya mbali kuuzuru mti mmoja uliopandwa miaka takribani thelathini nyuma. Walikwenda kwa awamu tofauti, na waliporejea wote, kila mmoja alitakiwa atoe ushuhuda.
Mtoto wa kwanza akasema: ameuona mti, lakini ulikua hauvutii; umepinda, mbaya na matawi yake yanayumbishwa na kutupwa na upepo.
Mtoto wa pili, akampinga mwenziye kwa kusema ameuona mti ni mzuri; umependeza una maua mazuri na majani ya kijani.
Mtoto wa tatu naye akasimama na kusema: ameuona mti.ulikuwa mbaya na umekauka...hauna majani wala maua.haukumpendeza
Mtoto wa nne aliposimama, akashangaa majibu ya wenzake.yeye akasema ameuona mti ukiwa umezaa matunda makubwa na matamu.mti ulikuwa ukinukia majani yaliyochanua.
Baada ya wote kutoa ushuhuda, baba akawaambia wanawe kuwa wote walikuwa sahihi, kwa sababu kila mmoja ameuona mti,lakini walitofautiana kwakuwa waliuona kwa misimu tofauti. Mmoja alikwenda wakati wa masika, mwingine wakati wa kiangazi, na wengine wakati wa kipupwe na mwingine wakati wa vuli.
Baba yao akawaasa kwamba, kamwe hawapaswi kuuhukumu mti kwa kuutazama msimu mmoja tu. Ikiwa leo umeukuta mkavu, usiukate, kwani msimu ujao utaukuta umeiva kwa kijani kibichi na matawi makubwa yatakayokufaa kwa kivuli. Na misimu mingine utaukuta umechepulisha maua na utafaidi matunda yake.
Vivyo hivyo, katika maisha tusimuhukumu mtu kwa kuangalia udhaifu wake mmoja tu kwamba ndio hafai kwa kila kitu....!
Ishi na mtu kwa kusoma nyakati zake..kila binadamu ana nyakati za hasira(mvumilie)..nyakati za shida na dhiki (mvumilie) ili uje kunufaika nae nyakati za furaha na mafanikio...!!.
Ukimhukumu mtu nyakati zake mbaya, hutamfaidi katika nyakati za utamu wake.Hakuna binadamu ambaye hafai kwa kila kitu.
Post a Comment