KWANINI UNA HUZUNI🤷🏽‍♂

Image may contain: one or more people
Wapi unahisi umekosea mpaka unapatwa na hali hiyo? Wengi wanaishi maisha mazuri kwa macho lakini mioyo yao imejaa huzuni, Wako ambao wanaogopa kusema wameshindwa tabia za wenza wao, Wapo wanao ogopa jamii pamoja na jamaa zao wasije kusema ndoa imemshinda, Je Mateso unayopitia wanaweza kukubebea japo kwa siku moja? Kwanini wao watake kujua uvumilivu wako lakini hawapo tayari kusikia umechoka na maisha hayo? Ndugu hebu wacha nikwambie:
"KUWA NA HUZUNI HAKUTAONDOA MATATIZO YAKO, LAKINI KUWA NA FURAHA KUTAKUPA NGUVU YA KUWEZA KUKABILIANA NA HALI HIYO" Unadhani kuna mtu atakuja mwenyewe kukupa furaha? Unatakiwa upambane💪🏽 mwenyewe kujiandalia ni namna gani unataka uwe na FURAHA! Ukijifungia ndani na kulia ndo mwenza wako ataacha kukutesa? Wapo walojiua kwa sababu matatizo yalipozidi hawakusema mwisho wao waliona ni heri kufa lakini aliyesababisha mpaka leo anaishi, Ya nini BP kwa mtu ambaye hajishughurishi na kuulinda MOYO WAKO? Hutamani kuanza upya kisa ULIISHAMZOEA? Mazoea yameua wengi, Mazoea yamewatesa wengi, Mazoea hayajawahi muacha salama mwenye nayo, Hebu ifikirie afya yako kuliko chochote, Yaani unataka KUFA KISA MAPENZI YA MTU MUONGO?
Waongo hawajui kuona huruma Kwani wao ni wabinafsi na mbinafsi hajali teso la mwenzie, Fungua MACHO utazame mbele, Kunjua MOYO wako aingie mwingine, Achilia MIKONO yako umpokee mwingine, Uvivu wa kufikiri UTAKUANGAMIZA.
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria 🤸‍♂


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post