KWANINI NI RAHISI KUWA NA MKE/MUME WA MTU NA USISIKIE WIVU?

Image result for sanchiworld
Sababu ni ndogo mno;
Wivu unatokana na UPENDO na kama unakutana na mtu anakwambia tayari yuko na mtu maana yake utakwenda kwenye penzi hilo ukijua ni la MPITO.
Ila kama unakutana na mtu anakwambia hana mtu maana yake utawekeza MOYO mwisho wa yote UPENDO HUSITAWI na kuleta taswira ya mazoea, kwa vyovyote vile wivu utatamalaki, Kwa hivyo mwanzo wa MAHUSIANO hayo ndio hubeba maana ya penzi lenu, Ni ngumu sana kukubari kuchangia ikiwa uliaminishwa uko peke yako, Kinacho uma ni namna ambavyo ULIMCHUKULIA MWENZA WAKO kwani anaeuma ni uliyemuweka moyoni, ila ambaye hakuwemo moyoni hata ukimkuta na mwingine wala hawezi kuumiza moyo, Kwa hiyo HUWEZI KUMPENDA MTU AMBAYE TAYARI ANA MWINGINE kwa sababu PENZI NI LA MMOJA NA MWINGINE ANABAKI KUWA DOWEZI.
Usimpende ambaye tayari aliiahapendwa Kwani huyo ATAKUUMIZA na mwisho wa siku utabaki kuwa mpweke, Muda ni rafiki mzuri sana kwenye maisha yoyote yale, Jifunze kuzizuia HISIA zako pindi unapobaini unatongozwa/unatongoza mke wa mtu, Kwake atakuwa nayo sababu ya kukupa nafasi JE WEWE UNATAKA NINI?
Watu wakiishakuwa pamoja kwa muda mrefu baadaye wakatofautiana USIAMINI KWAMBA HAWAPENDANI na pengine kupitia wewe ukarejesha penzi/ndoa yao kupitia wewe aliyesalitiwa akajua anataka kumpoteza mwenza wake niamini WATARUDIANA HUTAAMINI😅😅😅
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria💪


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post