KUNA WAKATI MAPENZI YANAWEZA KUKUFANYA KUWA NABII WA MTU ALIYESHINDIKANA;


Image may contain: 1 person, shoes
Wapo watu wameshindikana juu ya MAHUSIANO Yaani kila kukicha yeye ni kubadili wapenzi, Kwake kuacha ni kama kiu ya MAJI kwenye jua kali, Haoni shida kukuacha wala kuwa na mwingine Kwani HAJUI KUPENDA.
Hajui hitaji lake wala hajui Kwanini anahitaji, kwake MAHUSIANO ni kama dawa ya kutuliza MAUMIVU ama ni kama mkeka wakati ukitaka kunyoosha mgongo😅 Yaani yupo tayari kutumia gharama yoyote ili awe nawe kwa haja zake na pindi akiona humfai tena WALA HASIKII HURUMA KUKUACHA😭😭
Mtu wa aina hiyo ukimtuliza na akawa MWAMINIFU kwako Basi wewe ni NABII YAKE📖
Mtu aliyezoea kutanga na njia ukaweza kumfanya atulie kwa hakika wewe ni NABII wala huhitaji kujitangaza, Maana nguvu iliyoko ndani yako IMETENDA MEMA👏
Wapo watu wameshindikana, Yaani kubadili MAHUSIANO kwake ni kama kubadili shati wala haoni shida, Watu hawa wanapatikana sana kwenye NDOA ZILIZOKUFA ila wapo kulinda Mali ama Hofu ya jamii, kwamba watu wenye ROHO hizi ni MUME/MKE wa mtu ambaye anapitia magumu kwenye NDOA yake sasa anajaribu kujitengenezea AMANI kwa kuwa na mahusiano yasiyo na IDADI kwa kujaribu kuuponya moyo wake, Bila kujua kama anaumiza watu wasio na HATIA yeye kwa wakati wake anakuwa ameridhika, Ili akirudi kwenye ndoa yake awe na GANZI asitake PENZI WALA ATTACHMENT yeyote, Mara nyingi watu hawa ni wale WANAOPENDA KUABUDIWA ndiyo wenye vijitabia vya ubinafsi.
Wahenga walipata kunena;
"KILA SHETANI NA MBUYU WAKE"
Utapiga chenga sana ila mwisho wako ni kukutana na NABII WAKO huyo ndiye atakukwamisha na UTAKAA CHINI UTULIE.
Yanayokupa kiburi leo tarajia kutokukupa kiburi kesho, Kwa sababu leo yanaonekana kuwa na THAMANI lakini kila siku zitakavyokuwa zikisogea UTAYAONA YA KAWAIDA hivyo usijaribu kuharibu THAMANI YA UPENDO KWA MAMBO YA KUPITA kwa sababu YAKIISHA KUWA YAMEPITA UTATAMANI UPENDO huo ndiyo wenye nafasi MOYONI. Lakini ukiukosa huo WEWE NI KAMA MFU TU kwa sababu hutaona FURAHA YA DUNIA🌎
#Elista_Kasema_ila_Sio_Sheria🔨


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post