Sio ISLAMIC wala CHRISTIAN na hata zile NDOA zinazofungwa SERIKALINI pamoja na zile za KIMILA kikubwa itajwe kuwa ni NDOA.
Bora ufungwe miaka 30 gerezani kuliko kufungwa na kifungo cha NDOA iliyotamalaki MAJONZI japo kwa Mwaka mmoja tu😭😭😭
Mtu anafungwa GEREZANI kwa kosa, Maana yake itakuwa rahisi kwake kujutia kosa alilotenda hata KUFUNGWA KIFUNGO GEREZANI🔗
Lakini KIFUNGO CHA NDOA ni juu ya Maridhiano baina ya Mtu na Mtu kukubaliana kufungana na kuwa MWILI MMOJA kwamba hao watatengwa na KIFO
Jiulize baada ya KIAPO CHA HIYARI KWAMBA KWENYE NEEMA TUTAKUWA PAMOJA NA DHIKI ITAKAPOKUJA NITAKUWA NAWE ILI KUITIMIZA NADHIRI YANGU KWAMBA KIFO KITANITENGA NAWE👫
Hayo yote uliyataja na MUNGU aliyasikia, Maana yake uliweka AHADI MBELE YA MUNGU WAKO lakini siku zilivyosogea mambo yakaenda ndivyo sivyo hebu niambie UNAKIKWEPA VIPI KIFUNGO HICHO?
Ndani ya KIFUNGO CHA NDOA mfungwa hukosa japo ile hali ya MATUMAINI pengine Kuna siku atapata MSAMAHA kama ilivyo kwa KIFUNGO CHA GEREZANI Kwani Kuna wakati RAIS wa nchi anaweza kutoa MSAMAHA kulingana na Mamlaka aliyonayo, Lakini kwenye KIFUNGO CHA NDOA hakuna MSAMAHA wowote wala hakuna MBADALA WA UVUMILIVU zaidi ya kuendelea kutumikia KIFUNGO maana MUNGU anakataa KUACHANA isipokuwa kwa UZINZI.
Mpaka uje kuupata ushahidi wa UZINZI ni leo sasa? Wahanga wa kifungo hiki ni WANAWAKE mara nyingi Mwanaume anapohisi hawezi kuendelea na NDOA huwa hawatazami KIAPO NA KIFUNGO CHA NDOA zaidi wao huwaza zaidi KUWA HURU
Lakini Mwanamke anapokuwa AMEFUNGWA KWENYE KIFUNGO CHA NDOA ikumbukwe kwamba MWANAMKE akiwa kifungoni tayari anakuwa ameisha zaa na hilo ndilo limewapa WOGA wanawake wengi, akiwaza kwenda kuanzisha KIFUNGO KIPYA wakati tayari ndani ya kifungo alichopo KUNA UZAO WA MWANAUME ALIYEAPA KUTENGANA NAE KWA KIFO😭😭😭
Mungu awakomboe WAFUNGWA WOTE MLIOKO KWENYE VIFUNGO VYA HIYARI ZENU "ndoa" na ikimpendeza MUNGU AWAFUNGUE MINYORORO YOTE kwa uweza wake AWATETEE MNAOTESEKA KWA KUTIMIZA AGANO LAKE huku mkidanganywa na kuumizwa kwa UPENDO WENU WENYEWE😭😭
Ushushe UTUKUFU WA MUNGU kwa kutamka AMEN👏
HAPPY VALENTINE'S DAY 🌹🌷
#Elista_Kasema_ila_Sio_She
Post a Comment