Dunia inayo Mengi ya kukufanya utamani kufa ila baya zaidi ni pale MTU ANAPOKUFANYA PICHA YA MWINGINE🚸
Kwa sasa imekuwa kawaida wana mahusiano pamoja na wana ndoa kuwa na MBADALA.
Yaani mtu anagundua mahala alipo hakutakiwa kuwepo ila akashindwa kuondoka na badala yake kuendelea kuwepo kwa kutafuta MTU AMBAYE YEYE ATAKUWA KWA AJILI YA KUMPA AMANI BAADA YA UHUSIANO/NDOA ALIYOPO KUMNYIMA AMANI
Pengine ni kwa maslahi yake mapana JE HUYO ANAYEPEWA NAFASI YA MTULIZA STRESS ANAJUA NAFASI HALISI?
Maana kwa sasa kila unaekutana nae analia AMEUMIZWA na kunena mabaya tu ya mwenza wake, Ili anayesikiliza asikie HURUMA kitu ambacho baadaye kimegharimu wengi.
Kama MLINZI WA AMANI YA MWANAMKE AU MWANAMKE MWENZIO UNAJUA basi utakuwa na sababu zako ndo maana ukakubaliana na MAJUKUMU HAYO ili kumfanya Mwanaume/Mwanamke mwenzio abakie na NDOA YAKE.
Sina tatizo na ajuaye kwamba YUPO KWENYE PENZI LA MPITO ila ninamuongelea ambaye yeye kwa akili na moyo wake anaona AMEPATA na kumbe AMEPATIKANA😭
Huwa najiuliza swali moja bila majibu;
"HIVI KUNA HAJA GANI KUISHI NA MTU AMBAYE UNAAMINI HAYUPO MOYONI MWAKO?"
Kwa sababu mpaka mtu ukatafute mwingine maana yake UMEKINAI ama unaona hupati starehe halisi, Swali langu kwa watu wa namna hiyo;
▪KUNA RAHA GANI KWENDA KUCHEAT NA KURUDI MAHALA AMBAKO UMEONA HAPAKUFAI?
Mimi nadhani iko shida kwa watu wa aina hiyo, Maana kama umeona UHUSIANO/NDOA haikupi kile ulikusudia kujenga UMOJA na Mtu huyo kumbe unasumbuka nini na huko nje umempata ambaye unafikiri anakidhi vigezo? Mimi kama mpekuzi wa mahusiano nimebaini kwamba USALITI NI TABIA wala sio kitu mtu anajifunza, Maana kama angekuwa Mtu anajifunza kusaliti kwanini sasa HUKOMEI KUSALITI KWA MMOJA?
Maana Mtu akiishaanza kusaliti KAMWE HAWEZI ACHA kwa sababu moja tu;
"KIINI CHA USALITI BADO KINADUMU NAE"
Mahusiano ama ndoa sio VITU vya kulazimisha ni mambo yanayotokana na UHITAJI maana yake unayo hiyari kuendelea ama kutoendelea, Kujua tatizo la mahala ulipo halafu ukatafuta mbadala ili kupoza stress Kama wewe ni Mwanamke nakuita MALAYA
Kama wewe ni Mwanaume nakuita MHUNI
Kuna heshima kubwa Mtu akiijua THAMANI YAKE na kukataa udhalilishwaji wa ki UTU
Kuliko FEDHEHA ya kuitwa MALAYA ama MHUNI chukuwa uamuzi na ujue HITAJI LAKO HASA NI LIPI JUU YA MAHUSIANO AMA NDOA?
Usijaribu KUPOZA STRESS bali pambana kuhakikisha STRESS inakuondoka, Ndo maana nawasihi wanaotembea na WAKE/WAUME ZA WATU kujichunguza mara mbili mbili Kwani Mtu amemuacha mkewe/Mumewe nyumbani halafu anajifanya ANAKUPENDA Baada ya MDINYO anarudi nyumbani kwake WEWE UNAFAIDIKA NINI?
Fikiria zaidi kuwa mwenye KUIJUA THAMANI YAKO kuliko kuendeshwa na tamaa za ki dunia, Wanaume single wapo, Wanawake single wapo na kwa uhitaji wako USHINDWE WEWE TU
Kuliko kudandia WAUME/WAKE ZA WATU ukaishi kwa wasiwasi TAFUTA WAKO AMBAYE UTAKUWA NA SAUTI WAKATI UTAKAPOKUWA UNAHISI UNAIBIWA
Lakini wa mwenzio huna mamlaka nae utakuwa kama MBWA JALALANI kazi yako kunusa nusa wala hakuna chakula💃💃💃
#Elista_Kasema_ila_Sio_She
Post a Comment