Huu ni mfano ambao nautoa mara nyingi hasa wakawa wateja wangu, unapokua umeachana na mtu wako wa zamani na kukutana na mtu mpya mara nyingi watu wengi hutaka mahusiano yao kwenda harakaharaka, hutaka mtu mpya kuelekea kwenye ndoa au kama wanavyosema kuwa siriasi kuliko mtu wa zamani, hapana, haikua hivyo, hata kama ndiyo umetoka kuumizwa unatakiwa kujua mtu unayekutana naye ni mpya.
Atakutongoza au utamtongoza kama yule wa zamani, kwako wewe ni mpya na atafanya makosa kama yale ya yule mwingine, ingawa sasa hivi unatakiwa kuwa makini lakini usitake kumhukumu kutokana na yule wa zamani. Hutaanzaia pale ambapo yule mwingine aliishia apana, ataanza upya na kwake wewe ni mpenzi mpya, atafanya mambo yake kivyake na usitake aendelee alipoishia yule mwingine.
Kwa watu wengi hasa kwa wanawake wanataka mwanaume ambaye wanakutana baada ya kutumia muda mrefu katika mahusiano labda wamekaa miaka mitatu na mtu na kisha kuachana, utawasikia wanasema “Sasa hivi nataka mtu siriasi, mtu wa kunioa, sitaki mtu wa kunichezea.” Nikweli sikushauri utafute mtu wa kukuchezea lakini haimaanishi kwakua tu ulishatumia miaka kadhaa na X wako eti mpenzi mpya mtakaa miezi miwili na unataka ajitambulishe, hapana hakuna kitu kama hicho.
Sisemi utumie miaka mingine miwili au mitatu, hapana utakua ni ujinga na utazeeka lakini mpe muda wa kukujua na wewe umjue angalaua basi hata miezi sita umsome na kuona kama anaelekea, ukiona haelekei basi uulize na si kulazimishia, si kila siku kuulizia utakuja lini kwetu, utanioa na mambo kama hayo. Nilazima ujue huyu ni mpya, mnaanza upya na si kazi yake kuendeleza aliposhia yule mwingine.
Post a Comment