Vijana ambao hamjaoa au kuolewa tafadhali tafakari sana kabla ya kufanya na kufikia maamuzi ya ni nani atakuwa mkeo au mumeo. Uamuzi huu mmoja waweza kuwa asilimia tisini na tano ya furaha au maumivu katika kuishi kwako.
Baadhi ya vijana linapokuja swala la mapenzi, utoto umechukua sehemu kubwa sana, nd'o maana mabinti wengi wameingia kwenye mauhusiano na wanaume wenye kujitambua na nidhamu ya kila kitu na sio kutizama umri wala kazi.
Lengo la mahusiano sio kutembea mmeshikana mikono, ama kujipiga selfie pamoja ama kuvaa nguo za kufanana, hayo mambo ni ya vijana wadogo, hebu komaeni muwe na magari ya kufanana, mjenge nyumba nzuri, muwe na date nights, na msafiri pamoja around the world.
Na njia pekee ya kufanikisha hayo ni kama wewe na mwenzi wako mtaamua kufanya kazi kwa bidii huku mkimtegemea Mungu.
Share
Post a Comment