JINSI YA KUPUNGUZA UNENE KWA WADADA NA WATU WENGINE


No photo description available.
.Kwanza kabisa napenda kuwashauri watu wanene wasitumie vidonge/madawa ya kiwandani kwa lengo la kupunguza unene, kwani vidonge vina athari zake mwilini ukizingatia kuwa vina kemikali ambazo baadhi hubakia mwilini na kutengeneza sumu.Watu wanashauriwa kutumia vitamini itokanayo na matunda na mbogamboga. Aidha, kwa mtu mnene kushinda na njaa siyo dawa au tiba sahihi ya kupunguza unene. Mtu anayetaka kupunguza unene/uzito ni vema akazingatia misingi ifuatayo:*.Punguza kula chumvi nyingimaana chumvi inatunza maji mwilini ambayo pia yana mchango mkubwa katika kuongeza uzito wa mwili. Kwa kuacha kula chumvi nyingi maji yataweza kupungua mwilini kwa njia ya mkojo au jasho.*.Ongeza kula vyakula vyenye madini ya potasium, calcium, na magnesium ambapo madini hayo yanapatikana kutoka kwenye mbogamboga mbichi na matunda au maziwa ya soya.*.Kula vyakula vyenye wanga, punguza vyakula vyenye mafuta na protini.*.Kunywa maji mengi kiasi cha lita 2 kwa siku na kwa kila siku.*.Fanya mazoezi ya mwili/viungo japo kwa dakika 30 hadi 60 kila asubuhi. Kutembea ni mojawapo ya mazoezi.Katika kuongezea vitu hivyo hapo juu, mlengwa anashauriwa pia kutumia;*.Asali kijiko kimoja na kuchanganya nusu ndimu au limao kwenye maji yenye uvuguvugu kiasi cha glasi moja na kunywa mara kwa mara.*.Matumizi ya cabbage pia yamethibitika kuwa na mchango mkubwa katika kupunguza unene kwani kemikali zilizomo ndani yake zinasaidia kuzuia wanga na sukari kubadilishwa kimfumo na kuwa mafuta ambayo ndicho chanzo cha unene wa mwili.*.Ulaji wa nyanya fresh kati yamoja au mbili kila siku asubuhi kama kifungua kinywa kwa miezi kadhaa nako kunachangia kupunguza unene, na ni njia salama sana ya kupunguza unene.*.Kunywa glasi mbili za maji ya uvuguvugu kila siku asubuhi mara baada ya kuamka kunasaidia kupunguza unene.Aidha mtu mnene anaweza kutumia diet rahisi ifuatayo ili kupunguza unene;1.Asubuhi, kunywa juisi ya matunda fresh au kula matunda na kipande cha mkate usiopakwa siagi.2.Mchana, kula vegetable salad na slice 2 za mkate pamoja na matunda au juisi.3.Usiku, kula fruit salad au supu ya mbogamboga.Hakikisha ratiba hiyo inafuatwa kila siku na acha kabisa kutumia vyakula vingine vyenye asili ya mafuta kama vile nyama.Nadhani kwa hayo machache yanaweza kusaidia. Nimeona niwawekee diet ambayo ni rahisi kupatikana na kutengeneza kwa gharama nafuu.Asante.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post