JINSI YA KUJINASUA KWENYE PENZI LINALO KUNYIMA USINGIZI🤷🏽‍♂

Image may contain: 2 people, beard
JE UNAWEZAJE KUJINASUA KWENYE PENZI LINALO KUNYIMA USINGIZI🤷🏽‍♂
Ni kweli MOYO ukipenda unakuwa umependa but MATESO yanapozidi MOYO huo huo ndo wenye kuamua kuendelea ama kuacha, Kwanza kabisa fahamu jambo kubwa ambalo ndilo hula ufahamu hata kudhoofisha NGUVU YA MAAMUZI nalo ni;
KUMBUKIZI "memories" huyu ndiye adui mkubwa wa NAFSI
Nikiri kabisa UPENDO NI WA MMOJA lakini kuwe na utulivu wa penzi, Kama hakuna utulivu HIYO MAANA YA PENDO NI LA MMOJA ITAKUWA HAINA THAMANI! Watu wengi wamekuwa wakiyachukulia MAPENZI NI KAMA SIASA kwamba UNAAHIDI KWINGI ILA UTEKELEZAJI KIDOGO ili kumpumbaza mtu, Nirudi kwenye Maana ya ujumbe wangu;
Ni rahisi sana kuubadili UONGO kuwa UKWELI kuliko kuubadili UKWELI kuwa UONGO Mahusiano ni FARAJA🙋🏻‍♂ Mapenzi ni FURAHA NA AMANI kwa maana hiyo UKIKOSA FARAJA, FURAHA, AMANI huna haja ya kusema uko kwenye MAHUSIANO/MAPENZI/NDOA maana hayo ndiyo yawezayo kuujenga MOYO hata ukaijuwa THAMANI YA MWENZA WAKO👌
Kumbukizi ndizo zinazoweza kujenga BOND YA UPENDO ama kubomoa BOND YA UPENDO... Kwa maana hiyo Ukiona umepambana sana KUMLINDA mpenzi wako na unahisi ama kuona haendani na vile Unataka awe njia ni rahisi sana "FUTA KUMBUKUMBU ZAKE KOTE UNAKODHANI ULIHIFADHI, ACHA KUSIKILIZA MIZIKI AMBAYO MLIISIKIA MKIWA PAMOJA, USIVAE NGUO AMA VITU ALIVYOKUNUNULIA, USIPITE NJIA AMBAYO UNADHANI MTAKUTANA, EPUKA KUSOMA MSG ZAKE ANAPOKUTUMIA, CHAGUA MUDA WA KUPOKEA SIMU YAKE NA KUTOPOKEA" Na mengineyo yanayofanana na hayo🙋🏻‍♂
Ulinde MOYO usihisi UPWEKE kwa yeye kutokuwepo, Jipe ushindi kwamba WEWE NI WA THAMANI pamoja na kwamba uliyempenda ameshindwa kujua THAMANI YAKO💪🏽
Pigania AMANI ya nafsi yako kuliko hata STAREHE YA TENDO LA NDOA maana watu wengi akiona unampenda akili zao hufikiri ni mambo ya kitandani kumbe hilo ni jambo ambalo kwako wala hujawahi liweka kama kipaumbele chako, YAISHI MAISHA YAKUPAYO FURAHA kuliko kuishi kwa kudhani FURAHA ITAPATIKANA KWA NGUVU
Uwapo kwenye PENZI ni lazima upewe AMANI NA FURAHA Ukiona unapigania kupewa wakati ni sheria ya UPENDO kupewa hivyo vitu UJUE HAUKO MAHALA SALAMA
Panic at your own risk🙋🏻‍♂


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post