Jinsi Wanawake wanavyosababisha upungufu wa nguvu za kiume


Kesi ya wanaume kupungukiwa nguvu za kiume zimezidi kushika kasi, kiasi cha kufanya dawa za kuongeza nguvu hizo kuwa maarufu na zenye mahitaji makubwa katika jamii.
Waganga wa kienyeji wamekuwa wakitumia dawa hizo kama tiba ya msingi ya kuwavutia wateja kwenye biashara zao. Hii inaonesha kuwa tatizo hili ni kubwa miongoni mwa wanaume wengi katika jamii yetu.

Hata hivyo, utafiti unaonesha kwamba wengi kati ya wanaume waliowahi kutumia dawa za asili na zile za hospitali kuondokana na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume hawakufanikiwa kupata tiba ya kudumu, matokeo yake wamegeuzwa kuwa watumwa wa kila wanapotaka kushiriki tendo lazima wabwie ‘kolezo’ la kuwasaidia kuamsha hisia zao.

Kwa wanaume, ukosefu wa nguvu ni jambo linalouma na kuondoa kabisa ujasiri. Wengi kati yao wako tayari kutumia pesa na uwezo wao wote kuhakikisha kuwa heshima ya tendo la ndoa ikuwa katika miliki yao daima.

Lakini, watafiti wa masuala ya mapenzi nikiwemo mimi, tumegundua kuwa wengi kati ya hao wanaolalamika kupungukiwa nguvu za kiume, hawafahamu chanzo cha matatizo na namna wanavyoweza kuepukana na kasoro hizo.

Ushahidi uliopatikana kwa waathirika wa tatizo hili, unaonesha kuwa wanaume wanapokabili upungufu wa nguvu za kiume huishia kujuta na kujilaumu wenyewe bila kutazama upande wa pili wa washirika wao, namaanisha wanawake.

Zipo kesi za wanaume kujiua au kujinyofoa sehemu zao za siri kwa sababu ya kushindwa katika tendo la ndoa. Hali hii inatoa picha kwamba wanaume wengi hujitwika mzigo wa lawama wenyewe.

Dokta Bianca P. Acevedo kutoka Chuo Kikuu cha California, Santa Barbara anasema, wanawake huchangia kwa kiasi kikubwa tatizo la upungufu wa nguvu za kiume, jambo ambalo nami nalithibitisha kwa ushahidi wa kitaalamu ufuatao:


1: KAULI
Miongoni mwa mambo ambayo mwanaume hataki kuyasikia yakitoka kwenye kinywa cha mwanamke ni kuambiwa HAWEZI TENDO LA NDOA. Mwanamke akimwambia mwanaume wakati au baada ya tendo kuwa hawezi, atakuwa amemsababishia tatizo kubwa la kisaikolojia ambalo litampelekea kupotea nguvu za kiume taratibu.

Msaada unaohitajika kwa mwanamke anayekutana na mwanaume dhaifu kwenye tendo si kumwambia hawezi, bali ni kumtia moyo na kumsaidia kuweza. Wanawake wamewasababishia waume zao upungufu wa nguvu za kiume kwa kuwaambia maneno kama haya: “Yaani siku hizi sijui umekuwaje, yaani huwezi kazi kabisa!”

2 : UJUZI

Wanawake wengi hasa waliopo kwenye ndoa, wanapuuza ujuzi kwenye tendo la ndoa. Hawajishughulishi kumsaidia mwanaume ‘kuwika’, si wabunifu na watundu, jambo hili humfanya mwanaume kushiriki tendo kwa kutegemea kupanda kwa hisia zake mwenyewe, hivyo anapokuwa amechoka au ana mawazo, hawezi kusisimka kwa vile hapati ushirikiano toka kwa mwenzake.

Pamoja na wengi kutokuwa wajuzi, lakini wapo wengine ambao ni watundu mno kwenye sita kwa sita kiasi cha kumfanya mwanaume ajione kama mgeni wa mchezo huo.

Kimtazamo, wanaume hupenda sana ushindi wakati wa ‘kazi’, lakini pale wanapogeuzwa ‘chekechea’ hupunguza uwezo wa kujiamini na kuruhusu hofu kuongezeka mawazoni mwao, hivyo kuwasababishia tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Inashauriwa kwamba, mwanamke anapokuwa na uelewa mkubwa wa masuala ya mapenzi hasa wakati wa tendo, asioneshe kiwango kikubwa kwa haraka bali amchukulie mwenzake kama mwanafunzi, asiwe na maneno kama: “Leo nakuja kukupa vitu adimu kuliko vya juzi, hakuna kulala kasi mtindo mmoja.” Kauli hizi huwaogopesha wanaume na kuwafanya wapungukiwe na nguvu.

USAFI
Mwanamke anapokuwa si msafi, huweza kumsababishia mwanaume matatizo ya upungufu wa nguvu za kiume. Sote tunafahamu umuhimu wa usafi wa mwili na kero za uchafu wakati wa tendo, hivyo ni wazi kuwa mwanamke akiwa mchafu atamfanya mwanaume apoteze msisimko na uwezo wa tendo la ndoa. Unadhifu wa mavazi na mwili ni muhimu sana katika mapenzi.

GUBU
Jambo lingine linaloweza kumsababishia mwanaume upungufu wa nguvu za kiume ni gubu au karaha za maneno ya uchokozi yasiyokuwa na kichwa wala miguu. Uchokonozi wa mambo, ugomvi, usaliti na hali ya kutokuwa na staha ni mambo yanayosababisha tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

Mwanamke anapokuwa mwingi wa maneno ya kashfa, dharau na matusi huweza kumfanya mume amchukie na kutopenda kushiriki naye tendo. Uchunguzi unaonesha kwamba wanawake walioolewa wenye tabia hii, huwafanya waume zao wawe na msisimko wa kimapenzi kwa wanawake wa nje kuliko wake zao hao.

USALITI
Tabia ya usaliti kwa mwanamke ni chanzo kingine cha mwanaume kupata tatizo la upungufu wa nguvu za kiume. Mwanaume anapoona, kuhisi au kubaini kuwa anasalitiwa, huumia sana moyoni, maumivu ambayo hatimaye humfanya muhusika kuwa na mawazo mengi ambayo humuondolea hamu ya tendo.

Naomba nimalizie kwa kusema mada hii imezungumzia zaidi wanawake, lakini vipengele vilivyomo kwenye somo hili vinatumika pia kwa upande wa wanaume kuwasababishia wanawake matatizo ya kupoteza msisimko wakati wa tendo.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post