1. Akiwa na shida ya hela, hapa sio wote ila wengi wao wakiwa katika hali hii huwa anaejitokeza kwao na kuonekana anauwezo wa kifedha kuweza kukidhi haja yake au kumsaidia basi hicho ndio huwa kigezo chao cha kukubaliwa. Hapa mwanamke huweka pembeni vigezo vyote na kuangalia pesa tu.
2. Akifikia umri wa miaka 30 na kuendelea bila kuolewa, hapa wengi huwa na hofu KUU kuwa sasa usichana na ujana unakaribia kuwatupa mkono hivyo kutokana na uzuri wao kuanza kuyeyuka basi hujirahisisha mno kwa mwanaume yeyote atakayejitokeza na kuonyesha uhitaji. Hapa mwanamke hukubali kirahisi mno maana huona sasa mda wa kuchagua chagua haupo tena na uzee waja. Wengi huwaza NIKIZUBAA NANI ATANIOA NA UZEE HUU?
3. Akiwa mpweke - akiwa na kiu ya kuliwazwa kwenye upweke wake haangalii huyu ni mume wa mtu, mchumba wa mtu, mzazi wa mtu. Yeye anachotaka upweke wake uishe
4. Akiwa desparate (mwenye kiu ya kuolewa) - mwanamke akiwa kwenye hali hii, basi mwanaume yoyote kwake ni potential husband, awe mume wa mtu au la, akifikia hapa hajali mambo ya kupima afya, mambo ya dini au imani, vigezo na masharti vyote vinafukiwa ardhini.
5. Akiwa na kiu ya mtoto - Hapa hajaliwi mtu inajaliwa mbegu tu. Kila akiona mwanaume anamwona kama baba mtoto wake, hapa haliangaliwi penzi tena bali mbegu za mtoto. Hapa hata kama ana imani ya kuhamisha milima atakuwa tayari kwenda kwa mganga pale anapoona maombi hayafanyikazi. Mtoto atatafutwa come what may, come sun come rain.
UJUMBE: Hali yako na mapito yako yasikufanye ushushe standards zako. Ndio maana taji hata sikumoja haitolewi mwanzoni bali mwishoni. Yeye avumiliaye atavikwa taji.
#imepenya haijapenyaaa?
Nakutakia siku Njema Mungu Akubariki na kukulinda
🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼🙏🏼
Post a Comment