JE MOYO WAKO UNASEMAJE KATIKA HILO LINALOKUUMIZA LEO JUU YAKE?

 Image may contain: one or more people, people sitting and outdoor

Pengine woga ndo umetawala moyoni mwako, Pengine hofu imekujaa hata unakosa msimamo, Pengine unahisi huwezi kuishi bila yeye, Ngoja nikwambie sasa na ukiweza utapona kabisa japo kumsahau ndo itakuchukuwa muda, Nguzo kubwa kwenye MAUMIVU UNAYOWEZA KUPITIA KWENYE MAHUSIANO/NDOA NI KULIPOKEA TATIZO NA UKALIKUBARI... 

Hakuna kufa ikiwa utaijua sababu ya wewe kuwa kama ulivyo, Ni kweli amekuwa msaada kwako, Ni kweli amefanya mema mengi kwako, lakini kwa uhalisia wa MAPENZI HAYO SIO YALIYOKUPELEKA KWAKE wala hayawezi kuwa tiba ya hitaji lako juu yake na kosa lake kubwa ni yeye kudhani PESA zake ama hayo alowahi kufanya kwako ndo siraha ya kukutesa nayo, Pesa inaweza kununua kila kitu lakini haijawahi kuununua upendo wa dhati, Wema wowote ule unaweza ukatajwa kokote lakini wema usiotawaliwa na UPENDO huo sio wema halisi una unafiki ndani yake, Rafiki usiwe mjinga kukosa TUMAINI kwani leo yako haiwezi kuijua kesho yako, Kila siku inajitegemea kulingana na ilivyotajwa kwako, 

Huanzi wewe hata Mimi niliwahi kukumbana na hali hiyo lakini leo hata sura yake siikumbuki kwa sekunde mpaka niitengeneze ndo niweze kujua alikuwaje, Mtu anapotumia UDHAIFU wako kama kilema chako huyo hakufai na ukiweza kumuondoa naomba nikusihi USIKUBARI HUKO UENDAKO UKAJULIKANE MADHAIFU YAKO! Watu wengi hutesa wenzao bila huruma kwa kujiamini kwamba HUNA PA KWENDA sasa hebu muonyeshe kwamba HATA AKIJA AMBAYE HANA ELFU MOJA MNAWEZA KUISHI KWA KUCHANGISHANA KIKUBWA MKO NA FURAHA NA AMANI..

. Muachie UTAJIRI NA MALI ZAKE ili aendelee kuwanunua wenye MAHITAJI ya vitu vyake iko siku atakutana na wajanja wenzie AJUTIE wakati huo ninyi mtakuwa mlishashika kasi ya mafanikio, Kwani msingi IMARA kwenye mahusiano ni kunia mamoja, Inua ujasili uondoke hapo nina hakika safari yako ilisimamishwa tu ila Ulikuwa Bado Uko safarini mwisho unakaribia YUPO ALIYEANDIKWA KWA AJILI YA HAJA YA MOYO WAKO💪🏽
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria 🙋🏻‍♂


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post