HUWEZI KULAZIMISHA MTU AKUPENDE, ACHA UTAUMIA TU.

No photo description available.

Pengine mazoea yakakupa simanzi na kukukosesha amani, Kumbuka kuwa MAPENZI HAYALAZIMISHWI bali yanatengenezwa kwa hiyari, Ikiwa Umeshindwa kumsahau na unamkumbuka muda wote ni jambo jema JE UNAJUWA KAMA NA YEYE ANAIPATA HALI KAMA YAKO? Kumbuka mwenzio alijipanga kuondoka kwako ndo maana uliyaona yale, Kumkumbuka Sio kosa maana umekuwa nae muda mrefu Kuna mazuri alifanya kwako, kuna wakati ulishindwa lakini yeye alikupa nguvu, Kuna wakati alikufuta machozi kwa vilio vya maisha, USIMSAHAU... Lakini usijiweke kwake tena kama alishawahi kukuumiza atafanya hivyo tena, Niamini nilishawahi kuwa huko na niligunduwa kuwa MTU APENDAYE KUOMBA MSAMAHA SANA UJUE TABIA YAKE MBOVU hivyo alishajuwa udhaifu wako ni kukulilia huku akisema nisamehe, Atakutaka urudi mara nyingine Kwani anajuwa ulichonacho ambacho ndicho humrudisha baada ya kutanga na njia asikipate kwa ubora ule ulojaaliwa! Bado unampenda kwakuwa wewe hukupanga muachane na pengine hisia juu yake zutarudi ikiwa mtakutana JE UNAKUMBUKA SABABU YA YEYE KUKUACHA? Maana alisahau mazuri yako yote na alilewa Mapenzi yale ulimpa akajiona yeye ndo yeye hata akajikuta anakuumiza, Usimuwazie kama mtu sahihi kwako Kwani mtu sahihi kwako yuko nje huko... Endelea kutafuta! Kulikuwa na sababu ya mapenzi kuisha na yeye.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post