HIVI UNAJUA KWAMBA PENZI LA KWELI NI KIOO! UNAJUA KWANINI?



Image may contain: sky, cloud and outdoorPENZI LA KWELI NI KIOO! Yaani kila ukijitazama unavyompenda mwenzio unaliona pendo lake la dhati kwako... Hilo ndilo pendo ambalo unatakiwa utembee nalo, Yaani kila unapojaribu kuongeza kumpenda nae anakuwa na vitu vipya kwa ajili ya kukuonyesha kwamba ANAKUPENDA SANA! Mapenzi yametawala maisha ya kila bin adam aliye timamu, Ukiona unapendwa JIACHIE KWA MWENZIO ili ushuhudie kile kimeujaza moyo wake, Usichague mahala pa kumuonyesha mwenza wako vile ambavyo unajisikia vizuri uwapo nae, Mpe muda wako lakini pia akili yako isiwe na mwingine ili umtosheleze, Acha nikwambie jambo moja MAZINGIRA MAPYA HUSITAWISHA UPENDO kwa namna yoyote pendelea kuwa mbunifu wa location ili uweke kitu kipya ndani yake, Mapenzi yasokuwa na MUDA kamwe hayafurahishi Kwani kadiri mnavyokutana ndivyo mnavyojengana kuhitajiana, Ni shambani ama bustanini wewe mkubalie mkutane kikubwa UNAJENGA DHAMANA NDANI YAKE... Sasa wewe kaa ukiogopa watu ama kuwaonea aibu walimwengu aje ASHA/JUMA wampitie akajionee mambo MAPYA ubaki na historia uliwahi kuwa wake🤣🤣
Changamsha akili yako iweze kupambanua mambo kwa wakati niamini MAPENZI HAYAFI KAMA WENYE NAYO WANAYATIBU MAKOSA YAO!
#Elista_kasema_ila_Sio_sheria💑


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post