JE, YUPI NI MKE HALALI KATI YA KWANZA AMA WA PILI
Inamhusu kaka mmoja aliyekuwa ameokoka, alifunga ndoa ya kanisa na binti mmoja mpendwa mwenzake. Waliishi vizuri na mke wake lakini baadae walitofautiana baada ya mkewe kuchepuka. Kitendo kile kilimfanya mwanaume ajiskie fedheha sana na hatimaye akaamua kuachana na mkewe kwa sababu ya uzinzi aliofanya.
Baada ya mda fulani kupita yule kaka alipata mwanamke mwingine pale kanisani aliyekuwa tayari kumuoa. Alifurahi na kuamini kuwa amepata mwanamke atakayemfaa kuwa mke kwa mara nyingne. Walienda kanisani kufanya taratibu za ndoa ili ndoa ifungwe. Ilikuwa ngumu ndoa yao kukubalika kwa kuwa alikuwa ameshaoa mara ya kwanza hapo nyuma. Ila baada ya muda kidogo mchungaji pamoja na wazee wake wa kanisa walirizia ndoa ifungwe baada ya kujirizisha tena kwa maandiko kuwa ndoa ile ni sahihi ifungwe maana kilishosababisha yeye na mkewe kuachana ilikuwa ni zinaa. Ndoa ilifungwa na hatimaye yule mwanaume akapata mke kwa mara nyingine.
Baada ya muda kidogo kupita yule mke wa kwanza alirudi kwa aliyekuwa mumewe kutubu na kuomba warudiane, alilia sana na kusisitiza kuwa hapo mwanzo aliteleza na sasa amejirekebisha na ameshaomba msamaha kwa Mungu na anachohitaji kwa sasa ni msamaha kutoka kwake na kuomba warudiane. Kwa kuwa neno linasema samehe saba mara sabini, yule kaka alikuwa tayari kumsamehe ila alibaki njia panda na kushindwa kufanya maamuzi, maana alishindwa kujua yupi atakuwa mke halali kati ya yule wa kwanza ama huyu wa pili.
Hebu tusaidiane hapa, hii kesi inaamuliwa vip?
Post a Comment