HEBU SOMA KISA HIKIUTAJIFUNZA KITU

MBWA NA MFUPA WAKE!!
Kisa hiki cha Mbwa kimenikumbusha jambo kubwa sana katika maisha ya mwanadamu wa leo.
Gari dogo nililokuwa nimepanda tukielekea kwenye pilika za maisha ilikuwa speed kama 80/90 hivi....
Ghafla nikajikuta natamani ajitahidi kuongeza mwendo..
Mara gari lilipokuwa limekaribia kabisa Nikaona mbwa ameongeza mwendo ghafla na kufanikiwa kuvuka.
Pumzi ikanishuka na mapigo ya moyo yakaacha kwenda mbio.
Lakini kuna kitu tulikiona kimedondoka kabla mbwa hajavuka barabara.
Ndipo nikamsihi dereva turudi nyuma kidogo, ili tuone ni nini kilichodondoshwa na Mbwa.
Nilipoona kilicho dondosha nikajifunza somo kupitia kitendo kile
MBWA alikua amedondosha Mfupa uliokua mdomoni kwake.
Yaani Ilifika mahali mbwa hakuona tena thamani ya mfupa, aliona bora aache mfupa aongeze speed ili aokoe maisha yake mwenyewe.
Hii ni akili kubwa sana!!
Kuna wakati tukitafakari tunaona siku zinakatika, miezi inayeyuka na miaka inabadilika, umri unasogea lakini maisha yetu yako pale pale.
Yaani ulivyokuwa mwaka 2016 ndivyo ulivyo hata leo, hakuna kilichobadilika.
Kama ni uchumi hali ni ileile, kipato kiko palepale, ukitafakari sana unagundua hakuna kilichoongezeka zaidi sana hali inazidi kuwa mbaya.
Sasa utajiuliza kwanini kila kukicha afadhari ya jana unagundua kwamba kuna mfupa wa mwaka jana bado umeushikilia.
Kuna mfupa umeushikiria ndio sababu ya wewe kuwa hivyo ulivyo, sasa ili unusuru maisha yako unapaswa kudondosha mfupa huo.
MPENDWA ACHILIA MFUPA HUO.
KUNA MIFUPA UMEING'ANG'ANIA MWAKA 2019 NA HAUJAKUSAIDIA LOLOTE ZAIDI YA KUKUINGIZA KWENYE MATATIZO NA KUFANYA MAISHA YASIBADILIKE,
MWAKA 2020 TUSEME YATOSHAA.
Tukifanikiwa kuwa na ujasiri wa kudondosha mifupa hiyo, tutakua tumejiandalia 2020 yenye mafanikio.
Nina hakika imetukwamisha mno!!
HEBU TUFANYE MAAMUZI MAGUMU..
TUSIVUKE 2020 NA MIFUPA HIYO.
TUIDONDOSHE HARAKA SANA ILI KUNUSURU MAISHA YETU.
*Yamkini tumekuwa wepesi wa kulaumu na kunung'unika mbele za Mungu kuliko kuwa na mioyo ya shukrani hili nalo ni tatizo.
*Yamkini tumekua wazito kuthubutu na kuchukua hatua za mafanikio zaidi, huu nao ni mfupa.
* Yamkini tumekuwa mabingwa wa kutumia akili zetu wenyewe (Mbinu zilezile zilizotufelisha miaka iliyopita) pasipo kumshirikisha Mungu hiki ni kikwazo cha kufanikiwa kwetu.
*Yamkini tumekuwa waoga, tumejawa na hofu. Hatuwezi kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati sahihi huu nao ni mfupa mzito sana.
*Yamkini tumekuwa wazito kujifunza kutokana na makosa yetu na kuchukua hatua stahiki huu nao ni mfupa unaotesa wengi.
*Yamkini tunafurahia kuona wengine wanashindwa wakati tungeweza kuwasaidia na kuhakikisha wanainuka na kufanikiwa hili ni janga.
HII NI BAADHI TU YA MIFUPA TULIYO BEBA.
Hebu tuidondoshe mifupa hii ili 2021 tukawe mwaka wa kushuhudia na kushangilia mafanikio makubwa.
MUAMBIE JIRANI YAKO DONDOSHA MIFUPA INAKUCHELEWESHA.
Image may contain: 2 people, people standing


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post