HAYA NDIO MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU NGUVU ZA KIUME. - EDUSPORTSTZ

Latest

HAYA NDIO MAMBO KUMI USIYOYAJUA KUHUSU NGUVU ZA KIUME.

Image may contain: 2 people, people smiling, people sitting and stripes
Mtu mmoja aliwahi kuniuliza dokta kwanini unapenda sana kuongelea hizi maada za nguvu za kiume, nikamjibu kwasababu wahanga wa hili tatizo ni wengi kuliko jamii inavyofikiria ila kwa sababu ugonjwa huu hausabababishi kifo na ni siri ya kila mtu ndio maana jamii ina puuzia lakini kila mmoja anafahamu hali yake ikoje na mimi najua wako wengi na sitaacha kuwaambia na usipoyafuata nayosema hapa utakimbia ndoa au utaendelea kuadhirika kila siku jogoo anaposhindwa kuwika. hivyo siwezi kukaa kuongelea kuhusu vitu kama malaria wakati serikali na asasi za kijamii zingine kila siku zinaongelea habari hizo.
Nguvu za kiume ni janga kubwa ambalo linaitafuna dunia ya sasa na watu wengi wamekua wakihangaika huku na kule kutafuta dawa ya kudumu ya shida hii bila kua na ufahamu mzuri wa tatizo hili hivyo leo naenda kuwafunua akili watu wengi ili watulie nyumbani na waache kushinda kwa waganga wa kienyeji na kunywa dawa ambazo haziwasaidii kabisa.


Nguvu za kiume hupungua kadri umri unavyo ongezeka: homoni inayoitwa testosterone ndio inayomfanya mtu aitwe mwanaume yaani kwanzia sauti, kifua, na ukubwa na nguvu za kiume. Homoni hii hupungua umri unavyozidi kwenda na hili swala sio ugonjwa ni kawaida na sio kwa u-ume tu hata viungo vingine vya mwili huishiwa nguvu umri unavyosonga. Sasa mtu akifika miaka 35 au 40 anaenda kwa mganga anataka nguvu za kiume  zile za miaka 18, sio ugonjwa huo ni umri. Pia watu wenye umri zaidi ya miaka 31 wakishafika kileleni huchelewa kidogo kusimamisha uu-me kwa ajili ya kuendelea na raundi ya pili tofauti na vijana wadogo, hivyo suluhisho kubwa hapa sio kutafuta dawa za kuongeza nguvu za kiume bali kujifunza kuchelewa kutoa goli la kwanza ili umridhishe mwenza wako kwanza na kukubali ukweli kwamba umri umeenda. jifunze jinsi ya kuchelewa kufika kileleni hapa.


Huwezi kupona tatizo la nguvu za kiume bila kutibu au kujua chanzo chake: niliwahi kusema nguvu za kiume hupungua kwa sababu maalumu…. huweza kupungua sababu ya punyeto, msongo wa mawazo, kuchoka sana na kazi, maumivu makali ya mwili, magonjwa yanayoathiri  mishipa ya fahamu mfano kisukari na magonjwa yote ambayo yanakufanya usiwe katika hali ya kawaida humaliza nguvu za kiume. Bila kuacha kuatatua au kutibu chanzo cha tatizo huwezi kupona shida hii na itakusumbua daima.
Hakuna dawa ya kuongeza nguvu za kiume moja kwa moja duniani: dawa zote zinazotangazwa huongeza nguvu za kiume ni za muda tu na zingine sio za kweli kabisa ni za kitapeli tu,  baada ya dawa  ni zamu yako kuupa mwili vitu muhimu vya kiafya ili nguvu zile ziweze kua palepale ikiwemo kutovuta sigara, kunywa pombe kwa afya, maji mengi ,kupata hewa safi na kadhalika.
Ukiona kijana chini ya miaka 30 hana nguvu za kiume ujue sababu kuu ni punyeto; zaidi ya asilimia tisini na tano ya vijana wa chini ya miaka 30 ambao wanadai nguvu za kiume zinawasumbua sana ni kwa sababu ya kupiga punyeto kwa muda mrefu na mpaka sasa hivi bado wanapiga..
.punyeto humaliza nguvu vipi? Hamu ya kulala na mwanamke ni sawa na hamu ya kula, kama wewe muda wote umeshiba utakulaje? Hizo nguvu zinatoka wapi wakati wewe huna nyege hata moja? Acha punyeto na kama hujui jinsi ya kuacha soma hapa sio uendelee kusema hii ndio ya mwisho afu kesho unapiga tena.


Njia pekee ya kua na nguvu za kiume muda mrefu wa maisha yako  ni kufanya mazoezi ya kawaida na mazoezi ya  kuongeza nguvu za kiume: kama jinsi watu wanaofanya mazoezi ya mwili  wanavyokua fiti kwa nguvu na akili ni sawa na nguvu za kiume huwezi kushinda ndani kila siku kwenye mitandao ya kijamii na televisheni afu utegemee kupata nguvu za kiume wakati hata nguvu za kubeba kilo tano za sukari huna. Na hili ndio suluhisho pekee kwa watu ambao umri unaenda hakuna dawa wala miujiza ya tatizo hili, mazoezi ya viungo kama kukimbia, gym,kuruka kamba ni muhimu kwa nguvu hizo,lakini pia mazoezi maalumu ya uu-me ukiyafanya kwa uaminifu bila kukata tama hili tatizo utalisikia redioni na utafika umri mkubwa sana ukiwa bado uko vizuri.kama huyajui mazoezi hayo soma hapa…
Vyakula ni muhimu sana kwa nguvu za kiume kuliko watu wanavyodhani: kuna vyakula nilishawahi kuvitaja kwennye makala zilizopita ikiwemo ndizi mbivu, karanga, blue berries, kitunguu swaumu na chocolate.. utafiti unaonyesha kwamba wanaume wanaotumia vyakula hivi hua na nguvu sana za kiume kuliko wale wasiotumia. kuendelea kula vyakula ambavyo havina msaada kwenye mwili wako kama chips, soda, na mikaango mbalimbali hataikusaidia kwa tatizo hili zaidi ya kuendelea kuadhilika kila siku kwenye tendo la ndoa..


virutubisho vya maltmata vinaongeza nguvu za kiume; kuna dawa moja inaitwa malt maca imetengenezwa kwa mchanganyiko wa matunda, magome ya miti na mizizi, kiukweli dawa hii ni kiboko kwani imejaa vyakula ambavyo hata afrika hakuna na watu wote wanayoitumia kama chakula wanaisifu sana.dawa hii inuzwa na wasambazaji maalumu sio maduka ya madawa.


Unene na kitambi hupunguza sana nguvu za kiume na ukubwa wa unene: mwili mnene sana huleta uchovu mwingi na watu hawa ikifika usiku hua wamechoka sana na hawawezi kufanya lolote, lakini pia unene huo hufanya uum-e kufunikwa na mafuta mengi na kuonekana mdogo sana kuliko kawaida.hivo kama wewe ni mnene jitahidi lupunguza unene kwa njia zote ikiwemo mazoezi na kupunguza vyakula..


Uume kulala baada ya kufika kileleni haimaanishi huna nguvu za kiume; watu wengi huangalia video za ngono na kuona watu waliomeza madawa ya kuongeza nguvu za kiume wakiunganisha raundi ya kwanza mpaka ya tatu bila kuchoka  na kudhani ili ndio kawaida, hakuna mwanaume dunia hii anaweza kuunganisha raundi ya kwanza na ya pili kwani ile ni hali ya kawaida ya mwili wa binadamu[normal physiology] lazima uum-e ulale kidogo ndipo uamke tena.


Watu wa zamani hawakusumbuliwa sana na tatizo hili; maisha ya watu wa zamani kazi zao ilikua ni kama mazoezi kwao kwani zilikua ngumu na za kutoa jasho, chakula chao kilikua ni cha asili sana lakini maisha ya siku hizi ya kushinda umekaa ofisini siku nzima na kwenda kula na kulala jioni  lakini pia ulaji wa vyakula ambavyo sio vya asili havina msaada kwa mwili wako. Utakuta mtu anakula maharage ya super makert  afu yupo Tanzania, hivi kweli maharage ya kawaida sokoni yameisha au ni kutaka kuonekana na wewe ni wa kisasa?


Kuangalia picha na video za ngono kuna haribu sana nguvu za kiume kisaikolojia; miaka ya nyuma mtu alikua anaiona chupi ya mwanamke siku ya ndoa tu, na kweli mtu huyu anakua ni rijali kwelikweli, sasa siku hizi mtu unaenda kuoa umeshaziona chupi nyingi, video nyingi za ngono kiasi kwamba mwanamke akimvulia nguo haoni kipya kwake..achana na hizo video ili uwe salama.




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz