.. Hata Bikra Maria alitokewa na malaika wakimwambia atapata ujauzito kwa njia ya roho mtakatifu iweje wewe unayeshiriki tendo la ndoa na mwanamke halafu akinasa mimba useme ni bahati mbaya? Kuna makosa mengi wanaume hufanya kwa wanawake lakini kosa la kuikana mimba ama kumtenga mwanamke kipindi awapo mjamzito binafsi huwa nasema WALAANIWE! Kama kuna kipindi ambacho mwanamke huhitaji ukaribu wa mwanaume ni pale awapo mjamzito, Kwanza ngoja niwaambie wanaume wenzangu HIVI MNAJUWA NI JINSI GANI MWANAMKE ANAKUWA KIPINDI AWAPO MJAMZITO? Mwanamke awapo mjamzito huhitaji tendo la ndoa kuliko kawaida, Mwanamke awapo mjamzito huwa na joto zuri, Mwanamke awapo mjamzito humpenda mumewe zaidi ya sana laa kama ulimtwisha mimba mkiwa na ugomvi hapo bwana wengine huwachukia waume zao... Ni busara kwa mwanaume kuhakikisha anakuwa Karibu na mkewe ama mwanamke aliyempa mimba ili kumfariji Kwani MIMBA sio jambo dogo maana huchukuwa uhai wa wanawake wengi, Kuna wanaume akiona mkewe amebeba mimba husikia kinyaa na kumtenga kipindi chote cha mimba, Ki sayansi tendo la ndoa baada ya mimba kunasa ni muhimu sana ili kumkomaza mtoto na wapo wanaume wanajidanganya kuwa MWANAMKE AWAPO NA MIMBA HATONGOZWI weeee thubutuu yako siku hizi wako wanaume wanataka wanawake wajawazito tu hivyo jiangalie MTOTO atakomazwa na mwanaume mwenzio uje kuuliza mbona masikio sio yangu? Ha ha haaa.
Michezo, Matokeo, ajira, Livescore,msimamo wa ligi
Post a Comment