Dada, hivi unajua ukiwa smart kiakili unaweza jipatia mwanaume wa kukuoa humu mtandaoni? Naam, inawezekana, sema tu kuna mahala huwa mnakosea.
Unadate na mwaume inbox messenger yako, hata siku tatu hazijaisha unaanza kumuomba mara hela ya vocha, mara hela ya kusukia mara jino linaniuma unataka akutumie hela ya dawa, ama njaa inakuuma, unataka akutumie hela ya kula.
Dada zangu, hii tabia nawaomba kaka yenu muiache, inaweza kusababisha ukose mwanaume aliye siriaz. Si wote wanaokutongoza inbox yako ni wanaume malaya, wengine wanakuwa na nia ya kutafuta mwenzi wa maisha, ila kwa mwanaume muoaji akishaona unatanguliza sana hela mbele kuliko hisia zake, hakika hutamuona tena, badala yake wale wanaume malaya watakuwa ndo watawala wa moyo wako, matokeo yake unazalia nyumbani na mwanaume muoaji hayupo.
Kitu kingine ambacho nawaomba mjiepushe nacho dada zangu, usilaghai mwanaume akutumie nauri ilihali unajua kabisa akishatuma hutaenda. Una lengo akituma unakula nauri, na yeye unamblock, na huu nimechunguza ndo imekuwa mchezo wa dadaz wengi, mie kaka enu niwaambie, hii si nzuri, kwani inakutengenezea laana ambayo itakuwa inakutafuna taratibu. Huwezi jua mkaka wa watu alikuwa siriaz kiasi gani hata akakutumia nauri, huwezi jua mkaka wa watu kapataje hiyo hela hadi akahangaikia akakutumia wewe akiwa na matumaini makubwa huenda ndo utakuwa mkewe, ila unamtapeli, kadri atavyokuwa akisikitika, hakika na mambo yako hayataenda. Utakuwa ni mwanamke usie na mbele wala nyuma, unashangaa 'why' mambo yako hayaendi, kumbe umetapeli hela za watu waliokuwa siriaz nawe, hiyo tabia si nzuri dada zangu.
Ukiona mwanaume anaekutaka ni malaya, ana lengo tu la kukuchezea atimize ashiki za mwili wake, ni bora ukamwambia hauko tayari; narudia tena dadangu, kataaa hela yake na umwambie hauko tayari.
Nenda ikiwa umejiridhisha sera za huyo mwanamme kweli ana nia ya dhati ya kuanza maisha pamoja nawe baadae; nenda muonane na kwa karibu pia utaweza jiridhisha yuko siriaz kiasi gani huwezi jua kumbe utakuwa umepata mwenzi wa maisha yako kwa njia hii ya mtandaoni.
Mie nimewahi ona watu wamekutana fb na wamedumu kuwa mke na mme kwa miaka 10 sasa. Dadangu, ukiwa siriaz, uwezekano wa kupata mwanaume siriaz humu mtandaoni ni mkubwa sana, ila nikudokolee tu siri, ukitaka kumpata mwanaume siriaz muoaji, usiwe mwepesi kutanguliza mambo ya pesa, fanya penzi na hisia zake kuwa kipaumbele, nakuhakikishia, utajipatia mme bora humu humu mtandaoni. Kama umempenda na umejiridhisha ni mwanaume siriaz anatamani kuanza maisha nawe, akituma nauri nenda, natamani sikumoja ukiniita kaka yako ukiwa na kwako napata na pa kunywea chai njiani nikiwa na safari zangu.
By...
Kaka yenu, Isaya
Kaka yenu, Isaya
Post a Comment