Kama mwanamke kila unapopanga kuonana naye basi huja na rafiki yake au dada yake, kama kila unapotaka kutoka naye out kwanza huzuga zuga na kutafuta sababu lakini baadaye akikubali basi huja na rafiki zake. Lakini anaweza kuwa hataki kabisa kutoka na wewe out ila baada ya muda utakuta katoka na marafiki zake au anajisahau na kusimulia namna alivyotoka na marafiki zake.
Mbaya zaidi nikuwa anakuomba pesa za kutoka out lakini hataki kutoka out na wewe, hataki hata kuonekana mbele za watu na wewe, lakini basi hata kama ukifanikiwa ukatoka naye, ataka ambalimbali, hatataka ule ukaribu wa kuonyesha kama mko pamoja na kama ikitokea mtu ambaye hafahamu mapenzi yenu basi atakutambulisha “Huyu ni rafiki yangu anaitwa flani…”
Anakua na haraka ya kukutambulisha kama rafiki na hatajaribu kuonyesha chochote kama ni wapenzi. Lakini kama mmetoka na marafiki hata kama ni Club utafikiri wewe ndiyo shemeji, atakua bize na watu wengine hata kucheza na wewe hatataka. Wakati mwingine unaweza kumuambia tukacheze akakuambia sijisikii kucheza ila baada ya muda katoka na rafiki yake, au hata mshikaji wako wanaenda kucheza na ana enjoy.
Mara nyingi mkitoka pamoja na watu wengine atajitahidi kukaa kiti cha mbali kidogo na wewe. Ndugu yangu yaani kama bado unasoma na yote haya yamekukuta unafikiri nina habari njema kwanza nikupe pole. Huyo si mpenzi wako ni mwanamke ambaye anakutumia tu kwa wakati huo, kuna mambo mawili, kwanza inawezekana labda unampa hela, unamhudumia hivyo hawezi kukuacha.
Lakini kama huna hela basi jua kuwa anakutumia tu kwa muda, labda wewe ni mtu wake wa akiba, kwamba anakua na wewe kwakua ni mpweke wakati akikitafuta mwanaume mwingine wa kuwa naye. Au anakutumia kwa vikazi vidogo vidogo, kukutuma tuma labda kimapenzi kwa kupitisha siku, ila hata kama ni mkeo wa ndoa basi jua hakupendi, anakuvumilia tu kwakua hana mwingine akipata mtu wa ndoto zake atakuacha na huo wivu wako wa kudhani unammiliki!
Post a Comment