ALIYEACHWA AMA KUUMIZWA NDIYE ANAYEKUFAA ZAIDI IKIWA NAWE UMEJIPANGA KUINGIA PENZI LENYE FURAHA NA AMANI"

Image may contain: 2 people, people smiling, close-up

Kwanza naomba nikwambie jambo moja;
"ALIYEACHWA AMA KUUMIZWA NDIYE ANAYEKUFAA ZAIDI IKIWA NAWE UMEJIPANGA KUINGIA PENZI LENYE FURAHA NA AMANI"
Bwaga manyanga yako chini, Tupa vidumu na vibakuri ili UPEWE UPENDO💃
Hakuna aliyefurahia MAPENZI kwa kumpata mtu FRESH yaani ambaye ndo anayaanza mapenzi Wala hakuna aliye mwalimu wa mwenzie kwenye MAPENZI ila kila mtu hujifunza mwenyewe kutokana na MAKOSA AMA MAAMUZI YAKE💪🏽 Tambua kwamba hata Elimu haijengwi na Mwalimu mmoja, Mtu kufikia PHD ni mpaka awe amefunua vitabu vingi, Kuna wakati utajikuta huelewi unachokisoma, lakini unavyoendelea kusoma ndivyo ambavyo UTAJIKUTA UNAELEWA👌 Vivyo hivyo issue inayohusu MAHUSIANO/NDOA kwa ujumla na mapana yake huitwa MAPENZI ukomavu wake unaendana na namna ya MAPITO YAKO! Kwani mtu hujifunza kutokana na mwenendo wa uhalisia aliopo, Unaweza kuumiza wengi mwisho wa SIKU AKAJITOKEZA KIBOKO YAKO💃 Na hiyo ndo maana ya wewe kutajwa kuwa mwenye PhD💪🏽
Ni ngumu kuwa kwenye PENZI lililo na FURAHA NA AMANI ikiwa wewe mwenyewe huwezi kumpa FURAHA NA AMANI mwenza wako, Ukiona mtu anafikiria kukuacha ama ukaona matendo yanayoashiria kukuchoka ujue UMEMUONDOA KWENYE UPENDO na ndo maana anajaribu kujikomboa, Nikiri inaweza kuwa HASARA yenu wote ikiwa MTAACHANA MNAPENDANA
Hakuna Malaika kwenye MAPENZI sote tunaishi kwa kuzifuata NAFSI zetu japo huwezi kuwa na Mpenzi wako bila kupitia changamoto, Malezi na maamuzi kila mmoja na yake hivyo linaloweza kuwabeba ni UPENDO🤝🏼
Ili kupata idadi ya wangapi uliwahi kuwa nao kama wapenzi LALA KITANDANI TAFAKARI PEKE YAKO ukipata majibu inuka ujiangalie n then UJIJIBU MWENYEWE IKIWA KUNA FAIDA🙋🏻‍♂
Kuna starehe gani KUBADILI radha za wanawake? Je ni utamu ndo unaokupa kuendelea kuutafuta? Ama ni kujua size na kuongeza orodha ya wanawake?
Ingekuwa utamu unalinda MAPENZI wallah FANTA isingekuwa inakinaisha🤣🤣
Usimtazame mwanamke kwa matamanio kwamba atakuwa MTAMU HUYU Kwani UTAMU HALISI NI KUTOKANA NA VILE WEWE UNASHIRIKI NA MWENZIO💃
Mapenzi yanahitaji utulivu wa akili pamoja na kutomlinganisha mwenza wako na mtu mwingine, Ukipata BUSARA umemlinda mwenza wako🙋🏻‍♂


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post