1. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 40, waliosoma sana na waliosoma kidogo, wote wanakuwa sawa tu, ni wakati huu majigambo ya certificates, diploma, degree, masters, PhD, hupotea kabisa. Ni katika umri huu, inawezekana mwenye elimu ndogo, akatengeneza pesa nyingi sana kuliko mwenye elimu kubwa. Waliosoma sana na waliosoma kidogo, wote wanakuwa sawa tu.
2. Kama ulikuwa haujui, ikifika umri wa miaka 50, mtu aliyesemekana kwamba alikuwa mrembo, na mtu aliyesemekana kwamba alikuwa ana sura mbaya, wote wanaanza kuwa sawa tu. Ni wakati huu, mikunjo usoni, vipara kichwani, mvi n.k, haviwezi kukwepeka tena.
3. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 60, watu wanakuwa wamestaafu kazi, aliyekuwa na cheo kikubwa na aliyekuwa na cheo kidogo, wote wanakuwa sawa tu. Ni wakati huu, hawa watu wanakuwa washikaji, wanaanza kukaa kijiwe kimoja, wanapiga story zenye idea zinazofanana, mara nyingi utawakuta makanisani au misikitini pamoja.
4. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 70, mwenye nyumba ndogo na mwenye nyumba kubwa, wote wanakuwa sawa tu, wote wanahitaji nafasi ndogo sana ya kukaa, kwa kuwa ni katika kipindi hiki, kuhamisha-hamisha vitu, inakuwa taabu sana. Mwenye ghorofa atapenda kukaa nyumba ya chini, kwa kuwa miguu yake inaanza kukosa nguvu. Ni wakati huu, watoto huwaachia nyumba na kwenda kuanza maisha yao, hivyo, nyumba huwa kubwa kuliko mahitaji.
5. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 80, walio na pesa na wasio na pesa, wote wanakuwa sawa tu, hata mwenye pesa anapotaka kutumia pesa zake, anakuwa hajui wapi pa kwenda, wote tajiri na masikini, hubaki nyumbani tu.
6. Kama ulikuwa hujui, ikifika umri wa miaka 90, kulala usingizi na kuamka, vyote vinakuwa sawa tu, kwa kuwa hata ukiamka, unakuwa huna cha kufanya.
7. Kama ulikuwa hujui, baada ya miaka 90, masikini na tajiri, wote wanasubiri kifo tu.
Katika maisha, kama wewe ulidhani ni mtu muhimu kuliko watu wengine, kwa sababu either ya elimu yako, uzuri wako, nafasi yako kazini, nyumba yako kubwa na nzuri unayoishi, pesa au kipato chako kuwa kikubwa. Basi ulikuwa hujui tu, ila wee ni wa kawaida sana, hakuna mtu mwenye nafasi kubwa kuliko mwingine, ni suala la muda tu, hivyo tuishi kwa adabu.
Usisahau kulike, kocomment na kushare page hii!
Post a Comment