ACHA KUHUKUMU KABLA YA KUSIKILIZA;

 Utajua unalalmika sana na unaboa kama unamuona mwenza wako au mtu yeyote anafanya kitu flani, kabla ya kumsikiliza ili hata kama ni kukudanganya akudanganye ushaanza kumhukumu. Umemuona mpenzi wako anaongea na mwanaume au mwanamke, badala ya kuuliza unaanza nimekuona umesimama na Malaya wako, nishakuambia hiyo tabia yako, mfanyakazi mwenzako gani mnaangaliana namna ile.
Umekuta meseji “Mambo za tangu jana?”, unasikia “Mwanamke gani anakutumia meseji usiku huu!” Umemtumia meseji hajakujibu au unamuona online hachat na wewe unaanza. “Utakua ukichat na Malaya wako, usiku nimekutumia meseji hujajibu, kila nikiingia online unachat tu, kila saa simu yako iko bize ulikua unaongea na wanwake tu!” Humpi nafasi ya kujielezea ushahukumu, unakua na majibu yako kichwani na unaanza kulalamika.
Kama ingekua ni kuongea ungemuuliza mbona ulikua online hukujibu SMS zangu akakupa majibu kuwa labda alikua anachat kwenye group au alikua sijui anafanya nini! Lakini wewe unahukumu, unataja na Malaya wake na unaenda kuangalia na namba nyingine kuwa zipo Online unaamua kuwa alikua anachepuka. Amechelewa badala ya kusubiri aje akuambie kwanini kachelewa wewe anaingia tu ushaanza!
“Najua ulikua kwa wanwake zako, mtu gani unarudi saa nane, nimechoka kukufulia, atakua ni flani!” Simu inaita kapokelea nnje humuulizi kwanini ushaanza kuhukumu, “Najua ulikua unaongea na Malaya wako, najua hivi na vile!” Kama una tabia hizi, kama hivi ndivyo namna ambavyo mwenza wako akifanya kosa unaongea naye basi jua kuwa wewe huongei bali unalalamika.
Pia jua kuwa mwenza wako atakuzoea na hatakua akikuchukulia siriasi kwani hata wakati utakapokua ukilalamikia kitu cha kweli basi atakuona kama una kisirani. Nilazima ujifunze namna ya kuongea, kama unataka kuchukuliwa siriasi, kama unataka aache hiyo tabia inayokukera basi nilazima uache kulalamika na kuongea. Watu wanakuheshimu unapoongea zaidi kuliko unapolalamika.
Unaweza ukaona unaongelea kitu kila siku lakini wala habadiliki, kumbe ishu si kwamba hakusikii, hapana ishu nikuwa huongei bali unalalamika hivyo anakua anakuzoea na mbaya zaidi anachukulia kuwa kulalamika kwake si kwakua yeye anafanya makosa bali nikwakua wewe unakisirani. Hata akifanya kosa la kuonekana kwakua kashakuzoea ukiongea utasikia “Hiyo ndiyo kawaida yake!”
Idd Makengo


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post