Ziko sababu nyingi sana zinazosababisha ndoa kuvunjika.

Image result for MAISHA YA UPENDO YA MUME & MKE YANAJIONYESHA KWA MAMBO YAFUATAYO

NDOA KUVUNJIKA
Inategemeana na wahusika wenyewe. Kuna ndoa zingine zinavunjia ukisikia sababu uwezi amini ni sababu za kijinga kabisa.
Lakini Mimi nasema kila siku kuwa ndoa inajengwa, ndoa baada ya kujenga inatengenezwa

Mfano ujenzi wa nyumba
Kwanza uimara wa nyumba inategemeana na uimara wa msingi.
Aliyejenga kwenye msingi wa mawe ni tofauti na msingi wa matofari ya sument (block) pia ni tofauti na msingi wa matofari wa kuchoma pia ni tofauti na msingi wa matofari mabichi yasiyochomwa n.k

Lakini uimara wa msingi wa nyumba inategemeana na muda unaotaka nyumba yako idumu. Kama nyumba yako ni ya muda mfupi mfano mwaka mmoja, hakuna sababu ya kujenga msingi wa matofari block na sument lakini kama unataka nyumba IWE ya maisha yako yote na uwezo unao ni lazima msingi ugharamie sana.
Na kama unajenga jenga kiolela olela labla kwa kukwepa gharama basi uwe tayari kupokea mbaya kuhusu kuvunjika kwa nyumba yako.

Wapendanao wengi wanapotaka kuoana wanakwepa gharama mbali mbali, mfano gharama za maombi, ushauri kutoka kwa wazazi au viongozi wa dini au watu wenye hekima. Gharama ya kumwogopa Mungu wengi wako tayari kuvunja amri ya sita kuliko kumpoteza mpenzi feki. Gharama ya kufunga ndoa wanaona bora kuchukuana kiolela olela.

Hata kama nyumba umejenga kwenye msingi imara na finishing nzuri haina maana kuwa umemaliza kazi, ninaamini mara kwa mara utakuwa unaikagua nyumba yako na kuangalia sehemu yenye itilafu mfano bati kuvuja au ufa kwenye ukuta au langi kuchakaa n.k
Ili nyumba yako idumu muda mlefu lazima uifanyie ukalabati mara kwa mara, waswahili usema *usipo ziba ufa utajenga ukuta*

Vivyo hivyo kwenye ndoa. Ni lazima kuichunguza mara kwa mara ndoa yako kama kuna sehemu yenye itilafu mfano kuacha kuoga pamoja, kula pamoja, ukaribu wa kimapenzi, uwazi n.k
*usipo ziba ufa utajenga ukuta*

Kumbuka ni ngumu kuwa na ndoa TAKATIFU kama wewe mwenyewe hunakwepa gharama ya kuitunza ndoa.


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post