✋Jambo moja ambalo watu wengi wanaumizwa nalo katika mahusiano, ni kutokutambua hatma ya mahusiano yao. Kuwepo kwenye mahusiano bila malengo yoyote, Yaan wew umejiegesha tuu kwa mtu ili maisha yaendelee. Yatambue mahusiano bandia hapa.
👉Unaweza kuwa umeishi na kijana au bint katika mahusiano yenu kwa muda wa kipindi kirefu, Lakin hakuna hata mmoja wenu anaefahamu familia zenu, wala kufika. Hakuna hata mmoja kati yenu ametilia maanani suala la ndoa baina yenu au utambulishanaji, Epuka haraka haya ni mahusiano bandia, mahusiano haya hayana hatma juu ya maisha yenu lazima kuna mmoja wenu anataka kujichomoa lakin anatafuna namna ya kuzuga.
👉Aina nyingine ya mahusiano yasiyo na malengo ni hii, Mnaishi kweny mahusiano mda mrefu lakin kila ukimgusia mwenzio habari za kufunga ndoa, Anakwambia acha haraka, unapogusia swala la kuvishana pete mwenzio either kijana au binti mmoja wenu anakataa, mnapogusia suala LA kutambulishana mmoja analipinga na kuendelea kuvuta muda. Epuka mahusiano haya hayana malengo huwez kukaa na mtu kwa muda mrefu bila direction yoyote, mwisho wa siku anakua amekupotezea muda na malengo.
👉Kuna aina nyingine ya mahusiano unakuta baina yenu mmoja anajua familia yenu na mmoja hajui, Unakuta umeishi na mtu zaidi ya miaka 7 lakin hujui kwao, familia yao huijui wala hujawahi kufika, Ila kila unapomgusia akupeleke anakuwa mkali anakuzunguka zunguka au anakupiga kalenda kila siku, Ilhali yeye anajua kwenu, anaijua familia yako na . Epuka haraka kuna namna anataka akupwepe ila mpotezane lakin anatafuta mbinu ya kuchomokea, Ataendelea kukupotezea wakati kwa kukupiga tarehe mpk akuumize.
👉Usikubali kuishi muda mrefu na mtu asiyekubali kupajua kwenu, au kupajua kwako. Usiishi mda mrefu na mtu asiye na malengo ya mahusiano yenu, mtu asietaka utambulisho wa aina yoyote kwenye familia yenu Epukana nae asijekupotezea wakati, Usikubali kuishi na mtu Ili mradi siku ziende, Ishi na mtu kwa malengo katika mahusiano yenu.
J4REAL
Post a Comment