Unapoongea na wanawake wengi kuhusu kushika simu za wapenzi wao na kuwafumania wanakuambia “nakagua ili kupata ushahidi!” kwangu hiyo si shida shida inakuja kuwa unataka ushahidi wa nini?
(1) Umemchoka unataka kumuacha lakini huna ushahidi unataa ukishajua umuambie nimekuacha kwakua nilikuta meseji ya mapenzi?
(2) Unahisi anachepuka hivyo unataka ushahidi ili umuambie kuwa humuamini tena unataka mkapime na muwe umnatumia kinga?
(3) Unahisi ana mwanamke mwingine hivyo unataka ushahidi ili ujue kuwa ana familia nyingine usishirikiane naye kwenye mambo ya maendeleo uwe unafanya kivyako?
Unataka ushahidi wa nini? Wengi ukiangalia nikuwa, wanataka ushahidi eti ili mwanaume ajue nimejua, wanapenda ushahidi ili waombwe msamaha, eti kwakua kila siku mwanaume anakataa kuwa hachepuki basi wanataka ushahidi ili mwanaume akubali?
Akishakubali ndiyo nini? Akuombe msamaha wa uongo, apige magoti alie kama mtoto kukuomba msamaha wakati ni uongo wala hajajutia? Unaombwa msamaha lakini huwezi kumuacha, achilia mbali kumuacha hata kumuambia kuwa mkapime au mtumie condom huwezi msamaha unasiadia nini hapo?
Mwingine unamfuatilia, umejua, hata msamaha haombi ndiyo anapata uhuru kabisa wa kufanya mambo yake kwakua ushajua? Unamfumania anakuambia kuwa mimi nachepuka kwakua nataka mapenzi kinyume na maumbile utamuambia nini? Mwisho unasihia kuwa na kisirani, tu, unakua mtu wa kununa nuna kila dakika. Ishu iko hivi, unapokagua simu ya mwenza wako jua kuwa utakachokikuta ni kisirani chako.
Hata akuombe msamaha mpaka kulia hutakua na amani tena, lakini pia hata akaikuomba smamaha sio kwmaba ataacha kwakua umejua, sanasana atabadilisha mbinu na wewe utabaki na kisirani, mtu anaacha akijutia na akiamua, kama huna ubavu wa kumuacha au hata kumuambia mtumie kinga acha simu yake, kujua hakuwezi kukufanya usiambukizwe magonjwa kama huwezi kumuacha au kujikinga.
Post a Comment