WANAWAKE KUNA MAISHA BAADA YA UJANA, UMRI USIKUDANGANYE:


Ndugu zangu wanawake nataka niongee na nyie mambo machache, hasa katika umri wa ukuaji na ujanani. Nikweli ujana ni maji ya moto kawa wasemavyo wahenga ila ukiendekeze utaumia, Nikweli una hali ngumu kiuchumi lakin (Jali Utu Wako)...
👉Mimi sikukatazi kutumia mwili wako kama kitega uchiumi, Tumiwa tuu.
👉Sikukatazi kulala na wanaume kwaajili ya pesa, vipodozi, mavazi na hata magari. Lala nao tuu.
👉Endelea kulala na kila mwanaume unaemuona mbele yako, awe mfupi mrefu, mweupe mweusi, mnene au mwembaba. Endelea tuu.
👉Endelea kuweka rekodi ya kulalw kweny hotel kubwa like Ubongo Plaza, Sharaton hotel, Ostdrby street n.k.Endelea tuu.
👉Endelea kupanga idadi ya wanaume uliolala nao, mpaka iwe kubwa kuliko umri ulionao. Endelea tuu.
👉Endelea kujipa sifa kwamba umetembea na mume wa fulan na fulan ili kuwakomoa watu. Endelea tuu.
👉Endelea kuwachuna waume za watu ili wakupe pesa, simu za bei ghali, mavazi na misuko ya gharama kwa njia ya mwili wako. Endelea tuu.
👉Endelea na kauli zako za dharau kwamba "Its none of ur business" Nikweli hainiuhusu ndg yangu. Endelea tuu.
👉Ila utakapoanza kuona inanihusu ni pale utakapofungua mdomo wako na kusema, Unatamani mwanaume wa kukuoa akupende hivyo hvyo ulivyo, Pale umri wako utakapokuwa umeenda na umeshapoteza kila kitu hujabakiwa na chochote cha kusema utaringa nacho. Wala huna Jeuri ya kuchagua mwanaume kwako yeyote sawa.
Pamoja na yote hayo kuolewa utaolewa ila mungu lazima atakupa mwanaume wa kuendana na wew, Atakuwa alishafanya matukio ya ajabu na yasiyosimulika siku za usoni na huyo ndie atakuwa mumeo. Baada ya miaka miwili ya ndoa yako ndipo utakapo kumbuka kuwa kuna kanisa, na utaanza kuzunguka kwa kila mtumishi na kila kanisa ukitaka maombi maana yawezekana ulishapoteza kizazi chako ktk harakati za kutoa mimba ili kula ujana.
Nakusihi sana msichana usimdharau yeyote ambaye anasema na wew Ili kuokoa ujana wako. Wakati mateso yakizidi utakumbuka kuna mungu, nduguzo na hata marafiki lakin wote hawa hutapata mawasiliano nao sababu uliharibu kwa kiburi chako. Siku ukiona suala lako linatuhusu ndio siku ambayo muda wako utakua umekwisha.
J4REAL


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post