✋Hii ni kauli ambayo inazungumzwa na wanawake zaidi ya asilimia 96% katika midomo yao. Hata katika pita pita za wanawake utakapokua unaongelea juu ya swala la mwanaume utaskia unaambiwa hako kamsemo 'Wanaume ni watoto wa mama mmoja'.
👉Kiukweli Kinywa kinaumba na kuna kauliambazo zinaweza zikakufanya ubadilike kimaisha, au uonekane hivyo ulivyo miaka nenda rudi, Au Kauli hii ikunyime kupata kile unachohitaji kutoka kwa mwanaume ulie nae.
👉Wanawake wengi wanashindwa kuwa na stara katika kauli zao, Midomo yao imeumwa kwa kuchapisha maneno mengi yenye tija na yasiyo na tija. Kuna baadhi ya kauli ambazo zinaongelewa na wanawa.
👉Sikweli kwamba wanaume mama yao ni mmoja au kama tunavyomaanisha kuwa wanaume ni walewale, Sio kweli Kila mtu amezaliwa kivyake hivyo unavyoona mwanaume wako yupo ni tofauti na alivyo mwanaume wa mwenzio. Kama wew unapewa mia tano ya mboga, kwann umfananishe na mwanaume wa mwenzio asiepewa hata mia.
👉Mwanamke mwenzio anakwambia yan mme wangu ni bahili, hatoi pesa ya matumizi wala nn, Ukijiangalia ww unapewa pesa za mboga lakin ndio wa kwanza kuropoka 'Hawa wanaume ni mbwa au watoto wa mama mmoja'.
👉Mwanamke dhibiti kauli zako, mdomo wako unachapa maneno mengi kweli kweli, lakin ongea maneno yenye tija juu ya mumeo usije ukakosa matunzo kwa uzembe wako. Sio kila kitu anachoongea shogaa ako nawe una sapoti itakucost.
👉Ebu muone mumeo ni wa tofauti, mwenzio anapojaribu kukueleza juu ya udhaifu wa mume wake ebu tofautusha kabisa usianze kulinganisha na mmeo maana mwisho wa siku utabomoa nyumba yako kwa mikono yako mwenyew.
👉Jifunze kuweka tofauti kwa mmeo, teena usimfananishe na kiumbe yeyote, iwe kwa zuri au baya, bado havifanani lazma kuna utofauti tuu. Kauli ya Wanaume wote ni watoto wa mama mmoja itakunyima vitu vingi na kukivunjia mahusiano.
Post a Comment