✋Falsafa hii inamaana kubwa nataka wanaume mnielewe, Usimhukumu samaki kwa kushindwa kuruka hewani. Unajua Samaki ukimtupa ndani ya maji atakimbia mpk ushangae ila ukimuweka nchi kavu ili aruke utakua unamuonea. Ngoja nikutafsirie
👉Unajua kwenye maisha ya ndoa au mahusiano unaweza ukamdharau mpenzi wako alivyochoka na kuparara, Kwakua humtunzi kama inavyotakiwa basi unamuona mbaya wala hakufai, Inafikia hatua unamchukia kbsa mkeo au mpenz wako na kuanza kutaman wa nje kwa kuwaona ni wazuri zaidi..
👉Huyo mwanamke wako unaemdharau na kumchukia, ukamuona mbaya ameparara na kupaka. Nakwambia ukimuachia upenyo kidogo tuu akaenda kwa mwanaume anaejua kutunza haswaaa, Hakika utamsahau kama ni yule mchovu ulikua unaishi nae ndani, Ukikimbilia kumtelekeza na kukimbilia hao wa nje walio nawiri hakika utawachoka maana matunzo ni zero mwanamke anapendezea matunzo.
👉Ebu mfanye apendeze kama ww unavyopendeza, mfanye afurahie matunzo unayompa Unaweza ukawa huna pesa Bali ukimuonyesha upendo wa kweli, Hisia za karibu kwamba yes wew ndiye niliekuchagua kwa dhati ya moyo wangu matendo yako yatamnawirisha maana moyo wa mtu ukiwa umejaa faraja hata mwili nao hunawiri.
👉Nakwambia hivi hakuna mwanamke mbaya mbele ya matunzo, huyo mwanamke unaemuona mbaya akipata mwanaume mwenye moyo wa karakana zenye spear zote hakika unaweza kumsahau. Utajikuta unataka kumrudia ndio pale unaanza kuomba msamaha na ulishachezea bahati.
👉Niwashauri tuu wanaume weny tabia za kuwachukia wenzi wenu vile walivyo ebu wapeni matunzo muone watakavyokuwa soop, Usimlaumu mkeo kwa jinsi alivyo kwasabab hiyo nafasi aliyopo sio sahihi kwake, Ebu mtumbukize kwenye dimbwi LA matunzo uone anavyopendeza.
J4REAL
Post a Comment