Usije ukaoa Mapema kwa sababu hizi

Image may contain: 1 person

Usioe kwa sababu umechoka kula kwa mama lishe. Usioe kwa sababu umechoka kufua na kupika. Usioe kwa sababu rafiki zako wote wameoa. Usioe kwa sababu unataka kufungua kanisa sasa unatafuta mama mchungaji. Usioe kwa sababu wazazi wanakulazimisha maana dada zako wote wameshaolewa. Usioe kwa sababu mpenzi au mchumba amepata mimba yako. Usioe kwa sababu unataka kumuonyesha msichana aliyekuacha kuwa bado upo juu. Usioe kwa sababu unamhurumia msichana uliyenaye ukimuacha atachanganyikiwa. Usioe kwa sababu wazazi wako wanampenda na kumkubali msichana huyo.

Mke sio housemaid, kama umechoka kufua ajiri mtu akufulie. Mke sio mpishi kama umechoka kula kwa mama lishe jifunze kupika. Mke sio mashindano maana hataishi na marafiki zako wala sio zawadi kwa wazazi wako bali wewe ndiwe utakayeishi naye. Kuliko kumuoa msichana kwa kumhurumia na si kumpenda itapelekea kuteseka moyoni maisha yenu yote ni afadhali umwambie ukweli mapema.

Kuoa ili kujionyesha kuwa ume-move on baada ya kuachwa ni kujikomoa mwenyewe. Oa ukiwa na uhakika kuwa huyo ndiye chaguo lako pekee na upo tayari kuishi naye katika hali zote, ndio mpango wa Mungu katika maisha yako na ndiye unayempenda kwa moyo wako wote

Chris JR


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post