Vijana wa kiume, zunguuka dunia nzima huwezi pata mke mwenye busara, isipokuwa ni kwa Mungu aliye hai katika Kristo Yesu pekee, hata wazazi wako hawawezi kukupa mke, unaweza kupata mke lakini mke mwenye busara anatoka kwa Mungu (Busara ni kitu muhimu sana kwa mwanamke)
.
Swala la kupata mwenza wa kuishi nae ni swala zito kidogo, ambalo Mungu aliamua kulishughulia Yeye mwenyewe, kwamba ukitaka mke mwenye busara anakupa Yeye mwenyewe
Ikifika mahali unataka kuoa, kaa vizuri na Mungu, (Omba) mpelekee vigezo vyako unavyotaka angalia maono yako, alafu mwambie Mungu nataka mke wa namna hii, na Mungu kwa mapenzi yake atakupa haja ya moyo wako sawasawa na maono yako, ili yule mwanamke utakaepewa aje akusaidie kubeba maono yako
.
Mabinti - Usihangaike kutafuta mume, usitazame umri wala usisikilize maneno ya watu kwamba unatakiwa uolewe, wanakuharakisha bure wala usiwe na hofu
.
Kwasababu Wewe ni anaepanga utaolewa ni Mungu pekee yake, na Mungu ndio anakuletea mume, yani Mungu anatazama kijana aliyemuomba mke, akita kujibu atamuonyesha yule kijana kwamba huyu ndio mke wako, na wote mkikutana mtaona mioyo yenu inapata amani
.
Na binti ili Mungu akupe mume, inakupasa uokoke uwe ndani ya Yesu, kwasababu Mungu hawezi kumpa mtoto wake mke kutoka nje ya wokovu, Mtu akimuomba Mungu kwamba anataka mke, Mungu anaangalia ndani ya Kanisa, mabinti zake walioandaliwa na Mungu mwenyewe kuwa wake wenye busara.
Post a Comment