USALITI KWENYE MAHUSIANO..... - EDUSPORTSTZ

Latest

USALITI KWENYE MAHUSIANO.....

Image may contain: 1 personusaliti limekukuwa suala la kuumiza vichwa baina ya wapendanao. Asilimia kubwa ya watu walio kwenye mahusiano wamewahi kusaliti au kusalitiana.

Kusaliti hutokea pale mtu anapokuwa na uhusiano wa kimapenzi na mtu mwingine nje na yule aliyenaye. Wengi hufika mbali zaidi hadi kufikia pengine kuzalishwa au kuzalisha nje na mtu wake. Hali hii huathri sana mahusiano kwa kuwa kusaliti ni tofauti na kuachana kwani msaliti bado unaishi nae.
Ukweli ni kuwa usaliti huumiza sana kwan haufanywi na adui bali wapenzi, wake au waume tunao waamini sana hali ambayo hufanya msalitiwa kuumia zaidi...

KWANINI WAPENDANAO HUSALITI?
Kuna sababu tofauti baina ya watu zinawafanya wasaliti wapenzi wao. Nimekuwekea sababu hizo zisome hapaa.

1>> Tamaa kiukweli tamaa ndio chanzo kikubwa cha usaliti. Mwanaume kila akitembea hukutana na wanawake waliopendeza na hutaman pia mwanamke hukutana na wanaume watanashati na hutamani. Japo kuwa wanaume wamezidi sana katika kutamani kuliko wanawake.
Pia tamaa ya pesa hufanya mwanamke mpumbavu akaivunja ndoa yake kwa kuchepuka ili tu apate pesa. Kijana na mwanandoa chunga tamaa zako kwani usaliti ni mbaya uliyenaye ni mzuri sana ndio maana kuna mtu anamtamani kamwe usimdharau.

2>> Tabia za mazoea ndani ya ndoa na mahusiano... Hapa pamelate kizaa zaa. Uko kwenye ndoa ila unafanya vitu kwa mazoea yaani bora mradi tu basi. Kma huwajibiki vema basi jua mtu atafanya kila namna ili tu atimize furaha yake.
Unakuta mtu mara ya kwanza alikuwa anajituma kweli anajali kweli na anafanya kila kitu vizuri, ila kuzoea kuna fanya afanye mzaha ambao mwisho wa siku hufanya mtu asaliti...

3>> Kauli chafu na kukatisha tamaa, kila mtu anastahili heshima, je kauli zako zikoje? umekuwa mkorofi kwa mwenza wako unategemea nini akikutana na wanaojua kubembeleza? Lazima tu asaliti kumbe sasa ni kauli zako zinafanya mke au mume aone kama humjali...
Mke umekuwa na kauli kali mme anaona nyumba km kituo cha polisi ndio maana bora akacheze bao au kuangalia mpira

4>> Visingizio visivyo na msingi, mpo wote kwenye ndoa ila kila siku mke visingizio tu kila akitaka we visingizo akisema kiu cha ile kitu unasema anywe maji hapo akikusaliti usilalamike....... Pia mume jaribu kuwa muelewa ukiambiwa leo no usisaliti bwana..

5>>> Kuchokana pia ni tatzo, kipindi niko likizo babu aliniuliza wakati nmeenda kumtembelea likizo moja
*"et mjukuu unaweza kula maharage kila siku?*"
nilijibu *"kiukweli hapana babu maana hata huko shuleni nmeyachoka!
babu akaniambia mjukuu inawezekana kabisa kula maharage kila siku kwakuwa kama mpishi atatia viungo tofauti utahisi marahage ni mapya kila siku na hutayachoka hata siku moja!
babu alikuwa yuko sahihi kabisa na ndio uhalisia kuwa mbunifu kutakufanya usichokwe au msichokane...... Mapenzi sanaa kuwa mbunifu kamwe hata kusaliti....babu yangu ntakukumbuka......

6>> Ushauri mbaya na kuiga. kuna tabia za kuiga watu hufundishana kwenye vikundi huko sitaki kuvitaja, utasikia jiwe moja chungu hakiivi ama kizuri kula na nduguyo.... inakatisha tamaa ila epuka vikundi vyenye ushawishi mbaya na acha tabia za kuiga.....

7>> Kutoridhika na kutokuwa mkweli.. hii inahusu sana wale walio oana. Unakuta mke hajaridhika ila hasemi ukweli na anaamua kutafta mtu wa pembeni.sema ukweli ili mme ajue cha kufanya si kukaa kimya na kumsaliti. kuna njia za kumwambia sio kumkatisha tamaa na maneno ya shombo kitu ambacho mwanaume hukata tamaaa.. sema nae kwa upendo na atakuelewa msaidiane na huo ndio upendo

8>>zipo sababu. nyingine nyingi kama tabia ya mtu mwenyewe ambayo ni ngumu kubadilika na ndio maan kabla ya kuoa au kuolewa mtambue vema mtu wako.
jidanganye na kauli za watu et tabia tutarekebishana ujute. usifikiri ni rahisi kubadilisha mtu ambaye wazazi wameshindwa.....
mwisho
usaliti ni kitu kibaya huumiza sana na hata kama mtu atasamehe basi ni ngumu sana kuwa na imani na wewe kama ile aliyokuwa nayo mara ya kwanza...
plz usisaliti. comment like share ili watu wajue..




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz