UPENDO! Upendo ni nini?

Upendo ni UHALISIA wa nafsi kuwa na uhitaji wa kitu, Mtu ama jambo fulani,
Upendo ni UKWELI maana huko ndiko yalikozaliwa matendo yaponyayo moyo,
Upendo hautakiwi KUUMIZA maana sio tamaduni yake,
Unapompata mpenzi wako wa kweli usimuache aende mbali nawe mkiwa na migogoro,
Ukiwa na Mtu akataja UPENDO na kwa matendo akadhihirisha UPENDO wake kwako huyo ni wa kwako na ufanye unavyoweza kuhakikisha hatokei mtu akavuruga akili yake,
Unahitaji kuwapigania UWAPENDAO
Penzi halihitajiki kuharakishwa maana UPENDO halisi hujiendesha wenyewe,
Pendo linafanya kazi kwa nafasi yake, kama moyo wako umevunjika jifunze tu kuwa na furaha na ujipende mwenyewe wala usiwaone wengine kuwa kama wanahusika kukuvunja moyo wako,
Watu wanaweza kuwa wagomvi lakini PENDO lako likawaangukia bila wao kujua,
UPENDO NI UHALISIA basi uutafute uhalisia kwenye PENDO ambalo unadhani unalihitaji,
Ukiyumba ki fikra kwa sababu ya watu waliokuumiza hata ukaamua maamuzi mapya basi ujue unajiweka kwenye hatari ya kuikosa FURAHA NA AMANI ambayo umeijenga baada ya kuondoka huko ulikoumizwa,
Mapenzi ni kama tarehe kwani kila tarehe ina siku yake! Simama na mtu wako kwa hisia na akili ili usiishi kwa mashaka mwisho ukajikuta unaambulia maumivu yasoponyeka.
NINAJALI


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post