Unajua kuna aina fulani ya wanawake ukibahatika kukutana nao katika maisha yaani, unahisi umemaliza kila kitu aisee! - EDUSPORTSTZ

Latest

Unajua kuna aina fulani ya wanawake ukibahatika kukutana nao katika maisha yaani, unahisi umemaliza kila kitu aisee!

Unajua kuna aina fulani ya wanawake ukibahatika kukutana nao katika maisha yaani, unaweza jiuliza ulimpa nini Mungu mpaka akakupa bahati ya kuwa na mwanamke kama huyo.
Yaani wale wanawake ambao kwanza atakushangaza na uzuri alionao, pili atakakuvutia na hazina ya maarifa aliyoyajaza kichwani mwake, tatu atakuchanganya na maneno ya busara yatokayo kinywani mwake na mwisho atakuchanganya kwa namna alivyosafi kimwili na kiroho.
Nakwambia hivi, kuna baadhi ya wanawake ni moto wa kuotea mbali eiish!!! unakuta black sister anao uwezo wa ku-negotiate dili kubwa za biashara na wanaume wazito wenye mapesa na miguvu yao, lakini akirudi nyumbani kwa mumewe anakuwa mnyenyekevu mpaka unaogopa.
Black sister ameshika Dini ileile, ni mtu wa kusali lakini yupo romantic utafikiri alitoroka kwenye kambi ya waigizaji wa tamthilia ya TELEMUNDO. Yupo romantic kuanzia getini, bustanini, jikoni, sebuleni mpaka uwanja wa chumbani kiasi ya kwamba hutaki kusikia hata story za vinchenchede vya nje!
Hilo halitoshi, mwanamke anaendesha kikao cha bodi ya wakurugenzi wa kampuni yake, anakemea wazembe kazini lakini akirudi kwa mumewe ni mkimya, anamsikiliza mumewe anapoongea na wala sio mbishi.
Yaani unakuta black sister mzuriiiiiiiiiii kinyama, anavutia macho lakini anakuheshimu, anakujali na ni mwaminifu kwako,
Haya niambieni ukiachilia mbali mke wangu Nani mwingine mwenye mke Kama huyu...?




Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz