▪Mwanaume umuoe Mwanamke ambaye umemzidi Umri, Elimu, Pamoja na kipato ili ile hali ya UTII WA MWANAMKE ukadumu MAISHANI mwako ikiwa utajitenga na unyanyasaji kwa Mkeo na ukatawaliwa na HEKIMA.
▪Mwanamke uolewe na Mwanaume kwa UTASHI wake, Uwe na umri chini yake, Wala usilazimishe kuwa na kiwango Kikubwa cha Elimu zidi ya Mumeo pamoja na kusimama kwenye eneo lako kama MAMA itakupa kuepuka KUJIHESABIA HAKI na kumuona Mumeo ni Mtu tu.
Kwanza Wanawake wote mjue ujanja wenu ni kwenye USICHANA Yaani kabla hujazaa ila ukiishaitwa MAMA rafiki yangu kama hujajitambuwa MAISHA YAKO BAADA YA KUMKOSA ALIYEKUZALISHA AMA MZAZI MWENZIO ni sawa na Mpira wa kona Yaani kila mmoja anataka kuugusa😭😭
NDOA za namna hiyo nimeisema kwenye kichwa cha ujumbe wangu wengi wamedumu na kushiriki HESHIMA YA UPENDO kwa sababu Mume awapo kwenye kiwango cha hayo nilosema ni nadra Mwanamke kutomtii Mumewe, Lakini pia Mwanamke akiwa eneo lake nililolisema ni ngumu kwa Mwanaume kuhisi DHARAU kwa mkewe, Wanawake wengi mkisoma ama kuwa na hakika ya vijisenti mnataka kuwapanda vichwani waume zenu, Huku mkisahau akina BETINA wale wadangaji soko lao kuu WAUME ZA WATU wanaotaka FARAJA
Ndoa ni eneo TAKATIFU SANA japo wengi wamelifanya kama HAKIKA YA MATUMIZI YA MWILI kumbe ni HEKALU LA MUNGU.
Ili kuwa na NDOA IMARA kila Mtu na ajichunguze nafasi aliyopo na akatae ULINGANIFU⛔
▪Mwanamke mkatae Mume age yako, mishahara inalingana, Level moja ya Elimu Huko ndani mnakwenda kutengeneza BOMU likilipuka MWAFAAA😅
▪Mwanaume vivyo hivyo, Na kwako ni lazima uoe Mtu aliye chini yako ili kuweka HESHIMA KWENYE MAISHA YENU ile hali ya UFALME iwepo kwa wewe kumhudumia Mkeo na familia kwa ujumla vinginevyo UTAJUTIA.
Mwanaume DALALI huna Elimu, Mkeo ana PhD unategemea Kuna UTII utauona hapo? Ukiwaangalia wenye MAFANIKIO Kwenye NDOA zao unakuta BABA PROFESSOR na Mama Mwalimu wa msingi hapo UTII KAMA WOTE💃💃💃
Lakini pia niwakumbushe wanawake wote mnaotaka wanaume walio chini yenu ili kuwatawala MWANAUME NI MWANAUME BY NATURE anataka utii wako kwake, Kwa ujinga wake UTADUMU NAE ila mwenye akili itakuwa kama KUMPIGA TEKE CHURA eneo yalipo Maji atapendwa na Marafiki zako, Ndugu zako mwisho kabisa ATAKUACHA UKILIA kwa sababu wewe hukumtii.
Fuatilia ndoa za KUKURUPUKA ZINAVYOWATESA WENGI kila kukicha wakitafuta njia ya kuchomoka wala wasiweze, Ukiingia NDOANI umejinasisha mwenyewe UPAMBANE MPAKA KIELEWEKE😅
#Elista_Kasema_ila_Sio_She
Post a Comment