...
Nadhan siku zilizopita nilituma post ya jamaa kuomba ushauri juu ya amuoe nan kati ya mpenzi wake mpya (ambaye amemzidi umri ) au mpenzi wake wa zamani (anayelingana nae)
Sasa huu ndio mrejesho
Bwana fact baada ya kusoma yale maoni ya wadau wako nilipendezewa na maoni ya kuoa wake wawili
Sasa ikanibidi nikaongee na Yule Mama kwanza nimwambie ukweli kuwa mimi nina mpemz wangu na ninampenda ila nimeamua kuwaoa wote wawili na yeye atakuwa mke mdogo yaan nianze kumuoa yule msichana kisha ndio nimuoe yeye
Nilitarajia labda atakasirirka baada ya kumwambia hivyo lakin cha ajabu akabaki tu ametabasamu kisha ndio akaniambia kuwa ilikuwa anajua kila kitu kuhusu huyo mpenz wangu kuanzia jina, mahali anapokaa hadi namba yake ya simu anayo akanionyesha kwenye kikaratasi kidogo
Alisema kuwa hakutaka kuniambia kwa kuwa alihisi pangekuwa na ugomvi kati yetu hivyo akaamua kuwa kimya na suala la hiyo ndoa yeye amekubali kwa sabab yeye ndio amemkuta huyo
Kwa Mama likawa limeisha
Changamoto ikaja kwa mpenz Wang yule wa zamani baada ya kumwambia maneno yale akaanza kulia kwa hasira na kuniambia hawez kuolewa uke wenza na hata kama angeweza asingekubali kuolewa na mwanamke mwenye umri sawa na Mama ake
Hivyo ameniambia nichague moja kati yake au huyo Mama kisha akaondoka
zilipita siku tatu hapokei simu yangu wala Habibu SMS zangu namtumia whatsup anazisoma ila hajibu
Siku ya nne akanitumia sms Kuwa hataki mahusiano na mim tena na sasa hivi ameletewa posa nyumban kwao na amekubali kuolewa na mtu mwengine hivyo nimuache na nimsahau
Nimekutana na yule Mama nikamwabia ukweli wa yaliyotokea akaniambia hizo ni hasira tu ni jaribu kuzungumzia nae na nikishindwa niwakutanishe wote tuongee kwa pamoja jambo ambalo lilishindikana kabisa
Juzi nilimpigia Simu akapokea mama ake na kuniambia niachane na bint yake
Nimekata shauri la kumuoa huyu Mama baada ya kumwabia amekubali okay na yeye amenipa shart moja nimuoe yeye kisha nitafute mwanamke makamo yangu pia nione wawe wawili
Ameniambia kuwa nisipofanya hivyo ndoa yetu haitokuwa na amani kwa sababu naweza nikamletea maradhi na pia suala la uzazi linaweza likaleta changamoto
Mim nimekubaliana na wazo la huyu Mama na mungu akipenda kabla ya mwezi wa tatu mwanzoni nitaoa
Nimemuona huyu Mama anajua maisha na ananipenda na ameniruhusu hata nioe mke mwengine labda kama nikitaka kijana mwenzangu
Nimekubali kukabiliana na kila kitu katika maisha lakin huyu Mama amenitoa mbali sana kila nikijiangalia naona hatua zangu zipo na yeye
amenitoa kwenye uvulana na kuwa mwanume kamili ninayejielewa hata Mama yangu ananishangaa sana imekuaje nimebadikika tabia kwa speed kali Sana
Nakushukur kwa mawazo yako japo nilikusumbua kwa simu ila umenipa sapot kubwa ya mawazo pia wadau wako mungu awabariki
Nakushukur kwa mawazo yako japo nilikusumbua kwa simu ila umenipa sapot kubwa ya mawazo pia wadau wako mungu awabariki
Post a Comment