_UFUNGUO WA NDOA - SOMO LA 9⃣ >NDOA KATIKA DHOROBA<_*
🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝
🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝🗝
*_3⃣NDOA PASIPO MTOTO:_*
⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇
⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇⬇
➡👩🎤Dada mmoja aliyekuwa amedumu katika ndoa kwa miaka kumi pasipo mtoto, alikwenda kumfariji dada yake aliyekuwa amefiwa na mtoto wake wa tatu. Pamoja na kumfariji kwa mda mrefu pasipo kutulia alisema, *"laiti kama ingeliwezekana kwangu mimi kuzaa mtoto mmoja, hata kama angekufa bado ingekuwa faraja kubwa sana kwangu"!* Kauli hii iligonga masikio ya mama huyu aliyefiwa na mtoto wake na mara akagundua kuwa, *"utasa ni uchungu unaolemea.* Uwepo wa watoto unafanya uwepo wa jamii na taifa.
*_➡💜Mwanzo 1:28 Mungu akawabarikia, Mungu akawaambia, Zaeni, mkaongezeke, mkaijaze nchi, na kuitiisha; mkatawale samaki wa baharini, na ndege wa angani, na kila kiumbe chenye uhai kiendacho juu ya nchi._*
💠📌Changamoto ya kukosa watoto katika ndoa imedhihirisha tashwishi kubwa, si tu katika ndoa zilizotajwa katika Biblia *(Mwanzo 15:2; 30:1; 1 Samweki 1:6),* bali pia katika jamii mbalimbali za dunia. Mtazamo wa Wayahudi juu ya watoto ulikuwa mkubwa sana, maana watoto walifikiriwa kuwa, *"kizazi cha familia katika siku za usoni, na kwa sababu hiyo, kukusudia kutokuwa na watoto kulitamkwa kuwa ni dhambi kubwa."*
➡🕴🏽Josephus anasema, *Sheria ya Musa (Torati) ilikataza utoaji mimba, kuua watoto wachanga, au aina yoyote ile inayoharibu kiumbe na kupunguza binadamu.* Kwa Wayahudi, ndoa ilikuwa na kusudi moja kubwa, kuzaa na si vinginevyo. Si tu nyakati za Biblia, bali hata katika jamii za Kiafrika, kuzaa watoto ni tegemeo la kila ndoa. Kama John S. Mbiti anavyosema, *"watoto ni machipukizi ya jamii, na kila kuzaliwa na kuwasili kwa mtoto, ni 'majira ya kuchipua,' wakati maisha yanapo chipuka na jamii inaendekea kuwepo. Kuzaliwa kwa watoto sio tu shauku ya wazazi, bali pia ya jamaa wengi."*
➡Katika mtazamo huu, kukosa mtoto kunakuwa kama janga na msiba kwa ndoa husika. Biblia hutuambia kuwa, *_"Wana ndio urithi wa Bwana, uzao wa tumbo ni thawabu" (Zaburi 127:3)._* Kila mwanadamu anapaswa kuelewa kuwa uwezo wa kuzaa kamwe hautokani na mwanadamu bali na Mungu. Kwa bahati mbaya, baadhi ya wanadamu waliojaaliwa kuwa na watoto, kama ilivyokuwa kwa Penina na Hana, wanawabeza wanawake au wanaume wasio na uwezo wa kupata watoto, kanakwamba wao wanao uwezo au utaalamu jinsi ya kupata watoto hao.
➡Pamoja na ukweli kwamba panaweza kuwepo sababu za kibaiolojia au changamoto za magonjwa, kama sio kutokana na tabia zetu wenyewe zilizo sababisha utasa au ugumba, uwezo wa kupata mtoto anao Bwana peke yake.
*_➡💜Mwanzo 31:2 Yakobo akaona uso wa Labani, ya kuwa hakumtazama vema kama jana na juzi._*
*➡Ukweli huu unatuhitaji kuujua hasa kabla ya kuingia katika uhusiano wa ndia. Miongoni mwa mambo yatakiwayo kujadiliwa wakati wa uchumba ni suala la kupata watoto.*
🕴🏽🕴🏽Vijana wengi leo wameonekana kufaulu katika upande mmoja tu wa shilingi, kupanga idadi ya watoto wa kuzaa, lakini wanasahau upande mwingine wa shilingi - uwezekano wa kutopata watoti. Ni kitendo cha kishujaa kujadili na mchumba wako namna mtakavyoishi endapo ndoa yenu itakuwa mojawapo ya ndoa zisizobarikiwa kuwa na watoto katika dunia hii.
➡👫🏽🗝Ndoa nyngi zimevunjika kama sio kugubikwa na machungu, machozi, na simanzi, pale wanapokutana na uhalisia huu. Kwa kuwa baadhi ya wanadamu huchukulia utasa au ugumba kama aibu.
*_➡💜Mwanzo 30:22 Mungu akamkumbuka Raheli; Mungu akamsikia, akamfungua tumbo. [23] Akapata mimba, akazaa mwana, akasema, Mungu ameondoa aibu yangu._*
🗝Wengine wamejikuta wakikosa uaminifu katika ndoa zao, ilimradi wamepata watoto na wengine kuingia katika mitaala, pengine kutokana na ushawishi wa familia, marafiki, au wao wenyewe. *Waathirika wa hali hii wanahitaji upendo, huruma, na faraja toka kwa kila mwanadamu, maana hata hivyo hauna dhamana kwa watoto uliowazaa. Ziko ndoa ambazo licha ya kujaaliwa watoto wengi, zimekosa maziko ya watoto wao. Wazazi wanawazika watoto wao mmoja baada ya mwingine na kubaki kana kwamba hawakuwahi kuzaa. _>>>Itaendelea._*
🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒
📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌
🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒🍒
📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌📌
Post a Comment