UBORA WA NDOA UPO KWA WANANDOA WENYEWE





ni kosa kuitamani ndoa ya jilani yako kwa kuitazama jinsi ilivyo jaa amani nje ya kasha Kwani ndani ya kurasa wanaijuwa wahusika! Ni vyema kujifunza kwa wengine lakini pia usiamini kile unakiona nje kwani wapo wanandoa wanaishi kulinda watoto wao ama maliilopatikana wakiwa pamoja lakini walishatengana vyumba ila wakitoka katika geti moja ni ngumu kujuwa kama wana migogoro, Ni vyema ukajitathimini mienendo yako ili kama umekosea mahala uweze kujikosoa Kwani hilo ndilo litaipa NURU ndoa yako, Usiikinai ndoa yako kwa mambo yanayozungumzika maaana bila kusimamia maana halisi ya ndoa utajikuta UNAANZA KUTANGATANGA NA DUNIA ukidhani utapata nafuu na kumbe unabomoa MISINGI YA NDOA YAKO... Zungumza na mwenzio kila wakati, Usimpe nafasi akajiuliza na kujipa majibu mwenyewe nawe upo kwa ajili yake, Epuka kumuwekea mipaka mwenzi wako maana kuweka mipaka katika ndoa ni UBINAFSI na siku zote UBINAFSI NI UVUNJIFU WA AMANI.



0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post