UATESWA NA MAPENZI HEBU SOMA HAPA

Image may contain: 1 person, standing, close-up and outdoor

Huwezi kuyabadirisha yaliyokuumiza, Bali kupitia hayo unaweza kujivika ujasili kuendelea mbele hata kuufanya MOYO wako kurejewa na AMANI yake binafsi, Muda mwingine hatujui kwamba AMANI INATOKANA NA WEWE MWENYEWE kwa kushindwa kuweka uwiano baina ya HITAJI NA UHALISIA.
Unampenda mtu lakini yeye yupo kwako kwa mahitaji yake kamwe hamuwezi kusonga mbele, Unamhitaji Mtu kwa sababu zako lakini yeye anakupenda kwa vyovyote vile mtaishia kwenye ugomvi😭😭
Kwanza kabisa Kuna swali ni muhimu kujiuliza kabla hujawa tayari kumpa mtu nafasi;
"NINAMTAKA MTU WA AINA GANI?"
Kuna wakati unakutana na ambaye inawalazimu muwe wapenzi ila HAMPENDANI kutokana na UKARIBU pamoja na vile mtaonyeshana KUHITAJIANA mnajikuta mmezama penzini, Kumbuka huyo sio wa CHAGUO LAKO ila amepatikana kutokana na mazingira, Mlikuwa safarini ama ki kazi na wengine kampani ya marafiki inasababisha, Mwisho kabisa wa UHUSIANO huu ni pale atakapokuja MWENYE MAMLAKA KWENYE NAFSI YAKO hapo ndipo utajikuta njia panda😅😅
Uhusiano hata uwe mdogo kiasi gani kamwe ALAMA HUWA HAIFUTIKI kwa udogo wake Kuna jema ambalo litakufanya kulikosa kwa ambaye yeye ndiye unamuona sahihi kwako, Jambo moja nawasihi ni kujaribu KUYAKWEPA MAHUSIANO YANAYOTOKANA NA BAHATI MBAYA hayo yana gharama kubwa sanaa, Ili uishi kwa kuilinda AMANI YAKO BINAFSI unatakiwa kujuwa hitaji lako na kulipa kipaumbele na kwa kufanya hivyo utakuwa UMEIKOMBOA NAFSI YAKO💪
Yaliyopita yaache yawe kama fundisho, Anza upya japo ni ngumu lakini tambuwa kwamba;
KUANZA NI GHARAMA LAKINI UKIISHA ANZA UTATENGENEZA NJIA KUSAHAU YALIYOPITA NA KUBAKI KAMA SIMULIZI.
Gharama ya Maumivu ya MAHUSIANO inajengwa tangu mnapokutana, Yaani ule Mwanzo ndiyo unaoweza kuleta TASWIRA ya Mwisho wenu, Kuna wakati unahisi mambo hayaendi vyema ila ukajipa TUMAINI atabadilika hapo ndipo UNACHOCHEA MOTO🔥
Akibadilika MSHUKURU MUNGU ila kama itakuwa ndo mwendelezo wake wa kukupeleka KWENYE MAUMIVU rafiki huwezi kubaki salama
Inuka ujitetee binafsi yako ili ile AMANI itokanayo na wewe Mwenyewe iweze kufanya Kazi ili kukulindia MOYO WAKO.
#Elista_Kasema_ila_Sio_sheria🔨


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post