1.Mwanaume wa kuoa
Unapokuwa na mvulana ni rahisi kufikiri kuwa yuko sahihi, maana unakuwa kwenye mapenzi, kwa hio inakubidi kuwa makini kwa sababu kuna tofauti kubwa kati ya mvulana na mwanaume wa kuoa, ni kweli watu hubadilika kwa sababu mbalimbali.
kwa hio usiwe na imani kubwa kwa kuwa anaonekana kuwa na mapenzi mazito kwako, ni vizuri kumpa nafasi ya kujihakikishia kama kweli ana nia ya dhati. Na kama hutaona baadhi ya tabia zake kutokukupendeza , usisite kumwambia ukweli na kusubiri majibu yake.
Kama wewe bado ni msichana mdogo na ulikuwa unajaribu kujifurahisha katika maisha yako ni sawa kwa kuwa ni muda wa mpito, lakini kabla ya kupitiliza muda wako , utahitaji kutulia na mtu ambae ndio wa maisha yako. Kuna wasichana wazuri wanaojijali maisha yao , na hawapendi kupita huku na huku , hongera wewe kama uko kwenye kundi hilo. Kwa hio uwe na uhakika utafanya hilo kwa mwanaume mwenye sifa sio kwa mvulana mchanga.
Anapenda tu kutoka na wewe kufurahia na wewe , na huwa hawako tayari kuwajibika zaidi ya kukutaka kimapenzi, na baada ya hapo hukuacha mpaka siku anapokuhitaji tena.
.Mwanaume wa kuoa
Atakutaka uwe nae na utoke nae lakini ana kuwa na dhamira njema, kusudi jema, nia njema na wewe, kwa sababu anataka kuwa na wewe hapo baadae.na utamgundua tu toka mwanzo , maneno yake ya mwanzo huwa anamaanisha.
2.Mvulana unaetoka nae.
Atakuwa anaongelea kuhusu watu unaowafahamu kabla hujawa nae, na atakuwa anakuchosha na habari za mpira na ndondi , anatafuta story tu za kukufanya uwepo nae pale.
Mwanaume wa kuoa.
Huyu hushikilia maongezi yenye kujenga mahusiano, na hupenda kuleta mifano mizuri ya kwenye vitabu, movie,, music na mambo mengine ya kukufurahisha.hii inaleta kuvuta mahusiano yenu kuwa karibu zaidi na yataendelea mbele.
3.Mvulana unaetoka nae.
Atasema hataki kuoa na wala hataki watoto bado,na hakuna kitu kitakachombadilisha mawazo yake. Hapa usijaribu kumuomba kuolewa nae, hio ni bendera nyekundu imejitokeza, sio mwanaume huyo, sawa!
Mwanaume wa kuoa.
Mwanzoni tu huwa anaongelea habari za kuoa na kuwa na watoto, na wala hawezi kubadilika hapa.
Lakini naomba kuwekka angalizo hapa , sio wanaume wote wanaokuja na gia ya kuoa na kutaka watoto wanaoa, hapana. Usijirahisishe. Binti kuwa makini hapo.
4.Mvulana unaetoka nae.
Anaweza kusikiliza mtazamo wako, atachukulia kibinafsi, na ataanza mikwazo ilimradi tu mgombane msiendelee kuongelea mitazamo yako.
Mwanaume wa kuoa.
Anaweza kushughulikia mitazamo yako na kuongelea pamoja ili kuwekana sawa, na hii ni pamoja na kazi, na kama una maisha yenye mgogoro mkubwa au umekuwa na siku mbaya kazini kwako.
5.Mvulana unaetoka nae.
Atakuwa anakuita majina ya kitoto kitoto ili tu ajifurahishe yeye ndani ya nafsi yake, na kujiona kuwa ni mshindi.
Mwanaume wa kuoa.
Anapigania uungwana. Hawezi kukuita majina ya kijinga jinga,au kutumia nguvu ya mwili, haijalishi amekasirika namna gani, hujitahidi kuwa vizuri, kwa sababu anakuhitaji.
6.Mvulana unaetoka nae.
Hujali sana katika mwonekano, na atataka na wewe uonekane kama yeye, na mara nyingi anakuona hupendezi hiki jaribu hiki , hio ni kwa ajili yake. Atataka akufix atakavyo uwe katika ubora wake.
Mwanaume wa kuoa.
Anaelewa kila mtu ana siku mbaya na siku nzuri ,na anaelewa kuwa hayo yanapita, hawezi kukuumiza hisia zako au kuonyesha dharau kwako. Hata kama ulikuwa na mawazo mengi au nywele zako zimekaa vibaya, au umesahau kufanya usafi fulani kwa muda.
7.Mvulana unaetoka nae.
Atasema pole, samahani kwa sababu ni kweli ndio, na hawezi kuwa na maana ya kukuambia hivyo, yaani hamaanishi.hataki kukuudhi, anasema nakupenda kwa sababu hataki kukupoteza kwa maslahi yake, hata kama hajisikii kusema nakupenda , atasema tu mdomoni sio ya kutoka moyoni.
Mwanaume wa kuoa.
Atasema pole samahani, kwa sababu ni kweli anamaanisha hayo, na wala hana maana ya kukuumiza, maneno yake ni ya vitendo, anasema nakupenda kwa sababu ni kweli anamaanisha anakupenda, na atapenda wewe uhisi huo upendo kila dakika katka maisha yako.
8.Mvulana unaetoka nae.
Ana mategemeo ya kuona kila kitu kinafanyika, unamfanyia yeye, kwa sababu mama yake amekuwa akimfanyia . kupika, kufua, na inawezekana hata wasichana wengine wamemfanyia hivyo vitu, na huwa hajijali .
Mwanaume wa kuoa.
Anajua kujijali yeye mwenyewe, anajua kupika, kufua , usafi wa nyumba, kulipa bills n.k, kwa sababu amekuwa vakivifanya hivyo vitu kabla , na ndivyo alivyofundishwa.hiki ni ktu rahisi kujua ni aina gani ya mwanaume ulienae.
9.Mvulana unaetoka nae.
Hataki ukutane na marafiki zako kwa sababu anataka uwe nae muda mwingi umufanyie mambo yake.
Mwanaume wa kuoa.
Anapenda kusikia hadithi za rafiki zako na hata kutaka kuwaona na kuwafahamu.
10.Mvualana unaetoka nae.
Hawezi kukuchukua kwenda kuwaona wazazi wake, na hata ukimwambia kwenda kuwaona wazazi wako hataki , mnagombana kwa sababu ya hilo.
Mwanaume wa kuoa.
Atapenda kukutana na wazazi wako na kuwaonyesha jinsi anavyokujali na kukupenda, na atapenda kukupeleka kwao pia.
11.Mvulana unaetoaka nae.
Wewe ndio utakuwa wa kumkumbusha kuhusu kuoana nae, lakini yeye ataona kama unamsumbua akili yake, kwa kuwa anajiona yeye ni mzuri kuliko wewe. Na anaona yote ufanyayo ni kwa ajili ya kujifurahisha.
Mwanaume wa kuoa.
Kamwe hakuhakikishii kitu, wewe na yeye anaona mko sahihi , kama mtakaa na kujenga mahusiano yasio na mwisho, wakati wote yuko sahihi.
12.mvulana unaetoka nae.
Hakusikilizi , mara zote ni mabishano , huguna kila unapoongea, na mara nyingi hubadilisha mada , ili usimwelewe
Mwanaume wa kuoa.
Anajali unachotaka kuongea, anataka kujua mawazo yako na maoni yako kutokana na chochote ulichopitia kwa siku ile.
13.Mvulana unaetoka nae.
Hukimbia matatizo yanapotokea kwa sababu sio jukumu lake kwa maoni yake, na huwa hapendi kitu kimwangushe hasa .
Mwanaume wa kuoa.
Hushikamana nawe hata katika mambo magumu ya namna gani kwa sababu anaona ni jukumu lake kwako na mahusiano yenu. Na huwepo mpaka mwisho.
14.Mvulana unaetoka nae.
Hawezi kukusaidia hata kulipa bills, au chochote cha muhimu unapokwama, hata ukimwambia.
Mwanaume wa kuoa.
Analipa bills hata kama hukuomba kitu kwake kwa kuwa anafahamu majukumu, hata ukikataa atakusisitiza kuchukua.
15.Mvulana unaetoka nae.
Hana ulinzi wowote kwako, kwa sababu huwa hawazi nwala kufikiria wakati hauko nae, ana uwezo wa kwenda na marafiki zako ilimradi kujifurahisha. Hajali hisia zako.
Mwanaume wa kuoa.
Atakufanya ujisikie salama,kwa sababu muda wote utakuwa unajua kuwa anakupenda, utamthamini na kumwamini. Maana utajua kwamba wote mnajenga mahusiano yenye nguvu na kupita matatizo kwa pamoja.
Share this:
Post a Comment