Mama mjamzito alitoka nyumbani akaingia msituni kuchota maji kisimani, mara ghafla akaanza kujisikia maumivu sehemu za kiuno akaamua asogee kwenye kivuli.
Maumivu yalizidi kuongezeka na akaja kugundua kuwa ni uchungu na tayari alikuwa amefikia kujifungua. Aliangalia labda kuna mtu karibu aweze kumsaidia kwa bahati mbaya hakuona hivyo katandika chini nguo aliyo kuwa amefanya kama kata kichwani na kuanza kujifungua.
Alijitahidi akajifungua mtoto wa kwanza kabla hajapumzika akaanza kuhisi maumivu tena kumbe alikuwa anajifungua mapacha. Alijitaidi sana na kwa ujasiri mkumbwa akafanikiwa kujifungua mtoto wa pili.
Alipomaliza kujifungua nguvu zilianza kumuishia kwa mbali akamuona mwanaume akitokea vichakani akajua amepata mtu wa kumsaidia, mtu huyo aliposogea alionekana ameshikilia upanga mkononi kumbe mtu huyo alikuwa ametumwa na mganga wa jadi alete kichwa cha binadamu. Mtu huyo alipomuona huyo mama alifurahi na kujisemea kuwa dili lake limefanikiwa
Mtu huyo alimsogelea mama huyo na kunyanyua upanga juu ili amkate kichwa huyo mama. Kabla hajakatwa kichwa huyo mama na kugundua kuwa mtu huyo hana nia njema na yeye alifumba macho na kusema "MUNGU BABA MIKONONI MWAKO NAIKABIDHI ROHO YANGU."
Mtu huyo kabla hajashusha upanga, alisikia vitu vikikimbizana ndani ya kichaka kilochokuwa karibu na pale.. Ghafla vurugu kwenye shamba ziliongezeka na mara akapita Swala na nyuma yake alifatiwa na mbwa na zikasikika sauti za watu ambao walionekana ni wawindaji, mtu huyo alipoiona hali hiyo alitimua mbio na kutokomea porini.
Wawindaji walipomfikia mama huyo walishangaa sana na wakastisha kazi yao wakaamua kumbeba na kumpeleka hospitali. Mama huyo hakuamini alichokishuhudia akawa amebaki analia tu huku akimshkuru MUNGU kwa mema na makuu aliyomtendea mda ule. akawahishwa hospitali alienda kutibiwa mpaka hali yake iliporejea kuwa ya kawaida.
MWISHO.
ACHA MUNGU AITWE MUNGU, hawezi kukuacha kamwe. Kama unaamini sema Amen.
ACHA MUNGU AITWE MUNGU, hawezi kukuacha kamwe. Kama unaamini sema Amen.
#SHARE ujumbe huu mara nyingi uwezavyo na Mungu wetu wa Mbinguni atakubariki maradufu.
UBARIKIWE NA BWANA. 🙏
Post a Comment