Kuutunza MWANZO ni GHARAMA lakini FAIDA yake ni ADHIMU.
Kama kuna kitu kigumu japo kina manufaa ni KUUTUNZA MWANZO WA PENZI yaani ile TASWIRA ambayo iliwafanya wawili KUPENDANA hiyo ndiyo yenye MAANA ZAIDI kuliko hata UPENDO WENYEWE.
Kwa sababu UPENDO NI TENDO LA NAFSI na kwa vyovyote vile ni ngumu kujuwa kwa hakika ikiwa Mtu anamaanisha asemacho, lakini MATENDO YANALETA MAANA HALISI YA UJUMBE WA NAFSI kuliko MANENO.
Uzembe huanzia kwenye KUJISAHAU na mwisho kabisa UANGAMIVU HUINUKA KWA KUJIAMINI hapa ndipo Mtu anaweza KUMPOTEZA MTU WA MUHIMU kwa kushindwa kutambuwa kwamba;
"PENZI NI MFANO WA BUSTANI⛳ KWAMBA KILA SIKU LAZIMA UNYESHEE MAJI🚿" Unapoona PENZI LAKO LIMECHANUA🌷 ukajisahau na kujiamini niamini UKAME UTALIKUMBA PENZI LAKO na mwisho kabisa ni wewe kuingia kwenye MAUMIVU. Uliyoyatarajia YANAWEZA KUJA IKIWA UTAJUWA KUYALINDA lakini ambayo HUKUYATARAJIA HUJA KWA UJINGA WAKO MWENYEWE.
Utunze Mwanzo wa penzi lako ili ujiweke kwenye AMANI YA MOYO WAKO maana hilo ndilo chaguo lako, Lakini ukiona nakufundisha sana fanya kama hujaelewa namaanisha nini ili uje kujutia😅😅😅
#Elista_Kasema_ila_Sio_She
Post a Comment