NAKUFUNDA EWE MWANAMKE ULIYE KWENYE NDOA


Image result for tendo la ndoa asubuhi
Usinyanyue sauti mbele ya MUMEO kwa sababu yoyote ile. Hiyo ni ishara ya utovu wa heshima.

Usifichue udhaifu wa MUMEO kwa familia na marafiki zako. Itakurudia. Wewe ni mlinzi wa mumeo, naye ni mlinzi wako.

Usitumie mhemko yako hasi kuwasiliana na MUMEO, hujui namna MUMEO atakavyoitafsiri. Wanawake wenye hulka ya kujihami huwatengenezi nyumba yenye furaha.

Usimlinganishe MUMEO na wanaume wengine, hujui maisha yao halisi yalivyo. Ukiibomoa hadhi yake, upendo wake kwako utashuka.

Usimpe mtu mwingine fursa ya kumhudumia MUMEO, watu wanawaweza kufanya mambo mengine, lakini huduma za MUMEO ni jukumu lako mwenyewe.

Usiwe MKE mwenye matumizi ya hovyo mali, jasho la MUMEO halitakiwi kutumiwa hovyo.

Usijifanye kuwa mgonjwa kwa lengo la kumnyima tendo la ndoa. Mpe kwa namna apendavyo. Tendo la ndoa ni muhimu sana kwa WANAUME, ukiendelea kumnyima haitachukua muda mrefu kabla MWANAMKE mwingine hajatimiza jukumu hilo. Hakuna MWANAUME anayeweza kustahmili kukosa tendo la ndoa kwa muda mrefu.

Usiruhusu marafiki zako kuwa karibu mno na MUMEO.

Usimlinganishe MUMEO na MWANAUME wako wa zamani kitandani. Ukifanya hivyo, nyumba yako inaweza kupata mtikisiko wa aina yake.

Usisahau kuwa MUME anahitaji mtu anayemakinika naye na kumsikiliza vizuri, hivyo unapozungumza naye acha mambo mengine. Mawasiliano mazuri ndiyo msingi wa nyumba yenye furaha.

Usijibishane na MUMEO hadharani. Hilo litashusha hadhi na heshima yake. Hitajio namba moja la MUME ni heshima.

Usisahau kumuandaa MUMEO na kuhakikisha kuwa yuko maridadi kabla hajatoka nyumbani.

Wazazi au familia yako hawana uamuzi wa mwisho katika ndoa yenu. Endelea kuwaheshimu, lakini wasiwe na uamuzi wa mwisho kuhusu ndoa yenu.

🔴 NDOA IHESHIMIWE NA WATU WOTE 🙏 NA MALAZI YAWE SAFI 🙏


0 Comments

Post a Comment

Post a Comment (0)

Previous Post Next Post